Posts

Showing posts from August, 2023

144.Bwana, Bwana Ndiye Mtakatifu

1. Bwana, Bwana ndiye  mtakatifu,  anayo nguvu na sasa  aliyeko, na ajaye, Bwana! Bwana! Mungu, Mfalme, mwenye uwezo!  

143.Mungu ni wa Utukufu

1. Utukufu ni wa Mungu juu,  tukuzo lote, uwezo wote  ni wa Mungu, Bwana wetu, Bwana Wetu, Mungu ni wa pekee Shangilio lake Lijaze katika dunia popote, Jina lake litukuzwe  na watu wote.  Tumshangilie Mungu  wetu  na Bwana wetu nyimbo za tukuzo tumpeni heshima zote,  tumwimbie, Sifa na tukuzo zampasa  zote ni zake Mungu wetu!  

142.Vyenye Uzima Vimtukuze

1. Vyenye uzima vimtukuze,  vimtukuze Bwana,  vimtukuze, vimtukuze hata na utakatifu wake. Kwani ameumba  mbingu na nchi. Vyenye uzima,  vimtukuze,  vimtukuze Bwana,  vimtukuze Bwana,  vimtukuze Bwana, vimtukuze Bwana. Na magunda na mazeze  na filimbi na vilangwi  na vinanda  na vimtukuze! Vyenye uzima na viimbe  vimtukuze Bwana! Na magunda na vinanda  vyote vimtukuze Ee Bwana wa Majeshi! Haleluya!  

141.Tumpeni Sifa na Tukuzo

1. Tumpeni sifa na tukuzo,  sifa na tukuzo ni zake, Ukuu na nguvu  zote zimpasaye Mungu,  ni vya Bwana, ni vya  Bwana Na vimtii siku zote. 2. Tumpeni sifa na tukuzo,   sifa na tukuzo ni zake. Sifa, maombi na  nguvu zote ni za Bwana   siku zote,  kale yote  hata itakayokuja. Amen. Amen  

140.Tumsifu Sisi Watu

1. Tumsifu sisi watu,    tumsifu Mungu Baba,     aliyeumba vyote     kwa nguvu yake kuu.   Wazima watu wote,     na ndege wa angani     wanyama wa mwituni,       kwa huruma yake. 2. Tumsifu sisi watu,     tumsifu Bwana Yesu,     aliyetukomboa     kwa damu yake tu.    Amani tumepewa,     hatuna hofu tena    Ametuhurumia,    Mwokozi ni yeye. 3. Tumsifu sisi watu,     tumsifu Roho, ndiye     mtulizaji popote,      furaha iwe kuu.     Moyo umetulia,      amani umepata.    Awatakasa wote,      wamwombao yeye.  

139.Mungu Atukuzwe pekee

1. Mungu atukuzwe pekee,     shukrani zitolewe     sababu ya rehema kuu     aliyotutendea.      Mungu atupenda sana,      sababu hii ametupa       kutengemana vema. 2. Twakutukuza Baba mkuu       twakuheshimu sana,       sababu ya kutawala         zamani hata leo.        Nguvu zako haziishi        utakayo yatendeka,        Muumba wetu ndiwe. 3. Twakutukuza ee Yesu    Mwana wa Mungu wetu,    Uliyetupatanisha     na Baba mwenye enzi.  Mwana Kondoo wa   Mungu,   sikia tukikuomba  Mwokozi wetu ndiwe. 4. Twakutukuza ee Roho  uliyekuja kwetu. Uwape nguvu Wakristo  waliokombolewa. Utuokoe shidani. Shetani asitushinde, Mtuliza mioyo ndiwe.  

138.Tumepokea Neema

1. K: Tumepokea neema,          tuimbe sote kwa          shangwe. W:Tumepokea neema,        tuimbe sote        kwa shangwe K:Mungu Baba       Kampeleka      Roho Mfariji wake W:Mungu Baba        kampeleka      Roho mfariji wake. K: Ee ndugu, W: furaha kubwa K: isiyo W:na mwisho kweli K:Tunao W: sasa uweza K: kwa nguvu W: zake mwokozi. 2. K: Njoo, Roho mtakatifu,          utujaze nguvu zako; W:Njoo, Roho Mtakatifu,         utujaze nguvu zako; K: Tuende kwa watu       wetu,       tutangaze neema yako. W: Tuende kwa watu       wetu,       tutangaze neema yako. K: Ee ndugu,…. 3. K: Ee Roho Mtakatifu,             uliye Mwanga wa kweli,   W: Ee Roho Mtakatifu,  ...

137.Roho Wa Mungu Njoo Kwetu

1. K:/: Roho wa Mungu, Njoo kwetu, njoo, Roho wa Mungu W:Njoo kwetu njoo:/ K:Kanisani, W:Njoo kwetu, njoo. K: Kwa wachungaji, W: Njoo kwetu, njoo. K:Kwa walimu, W:Njoo kwetu, njoo K: Kwa waganga, W:Njoo Kwetu, njoo K:Kwa Wakristo, W: Njoo kwetu, njoo. 2. K:/: Roho wa Mungu,     Njoo kwetu,      njoo Roho wa Mungu, W:Njoo kwetu, njoo:/ K: Mashuleni, W: Njoo kwetu, njoo. K: Kwa wasichana, W: Njoo kwetu, njoo. K:Kwa watoto, W:Njoo kwetu, njoo. K:Kwa Wakristo W: Njoo kwetu, njoo. 3. K:/: Roho wa Mungu,     Njoo kwetu, Njoo Roho wa Mungu, W: Njoo kwetu, njoo:/ K: Shidani W:Njoo kwetu, njoo. K:Katika njaa, W:Njoo kwetu, njoo. K: Kifoni, W: Njoo kwetu, njoo. K;Furahini, W:Njoo Kwetu, njoo, K: Siku zote, W: Njoo kwetu, njoo 4. K:/: Roho wa Mungu, Angaza, uone ndani. Ya moyo wangu W: Angaza uone ndani:/ K:Kuna dhambi W:Angaza, uone ndani. K:Nyingi sana, W:Angaza, uone ndani K: Uniongoze W:Angaza, uone ndani K: Nitubu, W:Angaza, uone ndani K: Kwa faraja, W:Union...

136.Njoo Kwetu Roho Mwema

1. Njoo kwetu, Roho  mwema  Mfariji wetu. Tufundishe ya mbinguni,  tuwe watu wapya. /:Njoo, njoo, njoo, Roho mwema./: 2. Utufanye waamini     wa Yesu Mwokozi.    Tukaishi kikundini,      kanisani mwako.         Njoo, njoo, njoo 3. Kwa huruma tubariki,     tuishi na wewe,     tukatende kila kitu     tuongozwe nawe.          Njoo, njoo, njoo 4. Roho Mwema, Mfariji,     utupe hekima,    Tukiwaza na kutenda,    Yote yawe yako.    Njoo, njoo, njoo…. 5. Tudumishe, tuwe hai Na ukweli wako. Tusivutwe na dunia, Tushu’die neema. Njoo, njoo, njoo….  

135.Bwana Nasikia kwamba

1. Bwana Nasikia kwamba umebariki wengi nami nakuomba sasa: Nibariki na mimi! Na mimi na mimi Nibariki na mimi. 2. Nipatie Baba yangu, Kweli mimi mkosaji,  Baba uingie kwangu,  nirehemu na mimi! Na mimi na mimi Nirehemu na mimi. 3. Nipitie nakuomba, Bwana Yesu, Mwokozi,  wakosaji wawaita,  uniite na mimi! Na mimi na mimi Uniite na mimi. 4. Nipitie Roho mwema  kweli mimi sioni,  mwenye nguvu za kuonya, Nipe nguvu na mimi! Na mimi na mimi Nipe nguvu na mimi. 5. Nipitie Roho mwema  kweli mimi sioni,  mwenye nguvu za kuonya, Nipe nguvu na mimi! Na mimi na mimi Nipe nguvu na mimi.  

134.Njoo Roho Mwenye Uzima

1. Njoo Roho Mwenye      uzima, uliye Mungu kweli,     tujie na nguvu zako,     zituingie wote     ndipo na roho zetu      zitakapoangazwa. 2. Na mawazo yetu yote     uyajaze wema tu,     tusipende mabo yetu      ila mambo yako tu,     ujuzi wetu wote      ujae uzuri tu. 3. Wewe roho mwenye     nguvu,     na maonyo ya kweli.   Kazi zako ziendeshe     na kwetu sisi sote.   Utupe mata yako    tusikose kushinda. 4. Kufa kunapotujia,     wewe ututulize,     kwani tutapata kwako     utukufu wa kweli,     unaotuwekea,      wenyewe hatujui.  

133.Uje Roho Mwenye Neema

1. Uje Roho mwenye neema,      uje hua wa mbinguni,      lete mwanga wa upozi,      Ee mlinzi na kiongozi! 2. Tuchague njia yako,      kweli twaiona sasa,      ututie woga mwema,      tusimwache Mungu      wetu! 3. Tupeleke kwa Mesiya,     Yeye mwanzo wa uzima,       tuyatende mema yote,        ndiye njia ya mbinguni! 4. Tupeleke furahani,    tukapate kupumzika,    tupeleke kwake Mungu,    kwake iko raha bora!  

132.Roho Mtakatifu Wa Mungu Wetu

1. Roho Mtakatifu, Mungu    wetu,    mtuliza mioyo shidani,    watumwa toka mbinguni    na Mungu Baba na    Mwana,   Roho Mtakatifu mungu  wetu. 2. Roho Mtakatifu, Mungu    wetu,   uwashe moto wa upendo,  tupende Neno la Mungu  na kupendana na ndugu.     Roho mtakatifu… 3. Roho Mtakatifu, Mungu    wetu,    jaza tegemeo letu!   Pasipo msaada wa Roho    hakuna kutegemea. Roho Mtakatifu….. 4. Roho Mtakatifu, Mungu     wetu,     twaomba kwako ushujaa     wa kupigana na adui     mpaka tufike kwako juu.           Roho Mtakatifu…..

131.Siku ya Furaha (Tuliyoletewa Roho)

1. Siku ya furaha,  siku ya uzima,  tuliyoletewa Roho /:Yesu anatupa Roho Mtakatifu! Furahini!, furahini Wakristo!:/ 2. Siku ya furaha,      siku ya uzima,     tuliyoletewa Roho   /:Roho wa neema      ukatuongoze!     Furahini! Furahini      Wakristo!:/ 3. Siku ya furaha, Siku ya uzima,  tuliyoletewa Roho     /:Uingie kwetu Roho wa neema Furahini! Furahini Wakristo!  

130.Ee Roho Uje

1. Ee Roho uje, ee Bwana, Ujaze kipaji chako,  Kwao uliowakusanya   washa moto wa upendo! Umetuita mwangani,  tuwe umoja pendoni,  tulio wa ulimwenguni,   kwa hiyo daima twakusifu. Haleluya! Haleluya! 2. Mtuliza moyo Mtukufu,     tuagize, Neno lako     litufundishe kumtambua     Mungu na kumwita     Baba.     Umetuita….. 3. Vitani tupe upozi,     kituo cha kutulia,     na tusiogope ukali     wa adui na wa mwili    Umetuita…  

129.Twaomba Roho wa Mungu

1. Twaomba:Roho wa Mungu Mfariji wetu mkuu, Utupe baraka. Yesu alipotuaga, Kasema: Namtuma  Roho wangu kwenu. 2. Utuamshe wakosaji      kwa kuwa tu kondoo      waliopotea.     Uokoe ulimwengu,      umeharibika,      upate kujuta. 3. Roho wa ujuzi mwingi,     fundisha Wakristo     wampendeze Mungu.    Utufundishe kuomba      kwa Mungu vizuri,       tusikiwe naye. 4. Utusaidie sana,     tumshinde shetani     na dunia pia.    Tusitengwe na Mwokozi,     yakija mateso,     shida na huzuni. 5. Twakuomba uwe nasi     tulio wanyonge     tukijaribiwa.    Mwisho tuakapokufa,     tuone furaha     baada ya mateso.  

128.Roho Mtakatifu Uje

1. Roho Mtakatifu uje   utukalie na sisi,   fanya makao kwetu.    Utupe nuru ya mbingu,    ung’aze mioyo yetu,    tumtumikie Mungu.  Uje, lete utukufu   na furaha na uzima,    haya twafuata kwako. 2. U chem chem yenye rehema,     unatunywesha hekima,     watufundisha vema,      tujue kuwaambia      wenzetu wasiojua      habari za wokovu.      Roho zetu uzifanye,        tuyatende mambo mema        wewe utukuzwe sana. 3. Umande mzuri    wa mbingu     geuza mioyo yetu,     tujae pendo lako.    Tupendane na wenzetu,      tuwafanyie mema tu      na kweli watu wote.     Kwetu uwe upendano,      kugombana kuwe mbali,       tuwe na amani daima 4. Ututakase mioyo,  ...

127.Karibu Kwangu Roho

1. Karibu kwangu Roho    ingia moyoni,    uliyeniletea     uzima na raha.    Roho Mtakatifu     wa Baba na wa Mwana     ufananaye nao     ukaaye nao. 2. Unafundisha watu     kuomba vizuri,     wapate kusikiwa     na Mungu mbinguni.    Unatuombea,     hukomi, mpaka Mungu     atende mambo yale     uliyoyaomba. 3. Wafurahisha moyo,    hupendi huzuni,    tukiwa matesoni,    unatutuliza.   Wazungumza nasi     kwa Neno lako tamu,     unatia mioyo     furaha ya kweli. 4. Unatufanya sisi     kuwa usharika,    hutaki tugombane    na kuchukiana.   Wanaopigana    unawapatanisha,    wataka wapendane   Wakristo wowote. 5. Ulinde nchi yetu,    serikali yetu,...

126.Furahini Watu Wote

1. Furahini watu wote     furahini popote,     furahini wakosaji,     msifuni Mungu wetu.    Mtulizaji kafika,     aondoaye shida.    Nayo shida ikiisha     awapeleke mbinguni. 2. Amekuja nuru yetu,    Roho wake Mwenyezi,     awalinda watu wale     waliomtegemea.    Kila siku tusifu   neema yake na pendo.   Naye atatupa mambo     yafuatayo milele.  

125.Tazameni Anapaa

1. Tazameni, napaa,    mwenye kushinda vita,    gari lake ni mawingu,    ndipo anapopita,     malaika wa mbinguni     wakimwimbia Bwana,   Amekaribishwa sasa,     kwa kufurahi sana. 2. Ni nani anayepaa,     wote wakimsifu?   Ndiye Bwana mwenye    enzi,    ndiye Mungu wa Safu,      aliyeteseka kwanza      mle katika mti,      kwa kifo chake      mwenyewe,     akashinda mauti. 3. Akaaga watu wake,     na akawabariki    akapaa mawinguni     na wakimwangalia,   chini hutenda ya Mungu,     yote yakitimia,     kazi yake imekwisha,      kwake amerejea. 4. Ni kuhani wetu sasa,    yumo na damu yake,     katika patakatifu    twapatanishwa kwake,   Amefanya ukombozi    ...

124.Mbinguni Nani?

1. K: Mbinguni nani?  W: Mbinguni amepaa.  Ni Yesu Baba. K: Akawa wapi? W: Akawa kwa watu,  wamtia maumivu,  Akayalipa  Madeni makubwa,  na Mungu ampaza:  Aha! Mtawala! 2. K: Wenzangu nani?  W: Wenzangu waenda,  waenda mbinguni.  K: Na tuwe wapi?  W: Na tuwe kwa Yesu,   aliyetulinda.   Hapa duniani.   Sasa tunamsifu   Mwokozi wetu mkuu.   Aha, yuko juu! 3. Kuimba kwa kifukuzano  1. Mbinguni nani,  Mbinguni amepaa.  Ni Yesu Baba,  Akawa wapi,  Akawa kwa watu,  wamtia maumivu,  Akayalipa  Madeni makubwa,  na Mungu ampaza,  Aha! Mtawala! 4. 2. Wenzangu nani,  Wenzangu waenda,  waenda mbinguni,  Na tuwe wapi,  Na tuwe kwa Yesu  aliyetulinda.  Hapa duniani,  Sasa tunamsifu,  Mwokozi wetu Mkuu.  Aha, yuko juu.  

123.Siku Hii Tuliyomwona

1. Siku hii tuliyomwona akipaa juu mbinguni, alifia wakosaji, kurudia enzi yake. 2. Huko shangwe yake nyingi milangoni pa milele. Kashinda makosa, kufa, Yeye Mfalme mwenye nguvu. 3. Ajapokwenda mbinguni, alipenda ulimwengu. Akikaa kitini mwake, sisi atutunza hapa. 4. Tazama mkononi mwake alama za pendo lake! Awatia mibaraka watu na makundi yake. 5. Na sisi atuombea akikaa utukufuni, na atutengenezea  makao tukae naye.  

122.Shujaa Mkubwa

1. Shujaa mkubwa, Bwana wetu, leo umejikalisha kitini kwa Babako. Ufalme wote ni wako, umeshinda maadui, hawana nguvu tena. Umepewa enzi kubwa, kufa pia na uzima, vyote unavitawala. 2. Malaika wote wa mbingu wanakusifu kwa nyimbo wanakutumikia. Ulipotoka mbinguni ukaja kutuokoa, na umerudi leo. Sasa, wako utukufu; nasi tunakushukuru, tunasifu Jina lako. 3. Twataka kutafuta tu ufalme wako wa mbingu. Utupe nguvu zako, tushike mwenendo  mwema, tusiwe wenye kiburi ila wanyenyekevu. Tuepuke kila kosa, tufuate njia yako ya kuingia mbinguni. 4. Yesu mwana wa Daudi uliyetupatanisha na Bwana Mungu wetu. Ulipokwenda mbinguni umetutengenezea makao ya milele. Tuongoze, tusichoke, tusafiri siku zote; kwani watungoja kwako.  

121.Mwokozi Wetu Amepaa

1. Mwokozi wetu amepaa mbinguni! Neno hili linatufariji sasa katika woga wote. Kikiwa kichwa mbinguni, hata viungo vyafika alikokwenda yeye. 2. Mwokozi wetu amepaa mbinguni, mwenye nguvu. Mbinguni nitapokewa nitengemane kweli. Sababu hii ninataka kufika pale alipo Mwokozi wangu Yesu. 3. Mwokozi wetu amepaa mbinguni! Nakuomba: Bwanangu nisaidie nikutegemee wee. Nikufuate daima, mwisho nifike kwako juu nikiacha dunia.

120.Ameingia mbinguni

1. Ameingia mbinguni. Haleuya Kristo mwenye utukufu. Haleuya. 2. Akaa kitini kwa Mungu Haleluya! Mkuu wa dunia na  mbingu. Haleuya! 3. Sasa limetimilika. Haleluya! Agano lote la kale. Haleluya! 4. Mwana Daudi, Mfalme     mkuu. Haleluya! Sasa ni Bwana wa wote. Haleuya! 5. Sababu hii tumsifuni. Haleluya! Yesu Mwokozi wetu  mkuu! Haleluya!  

119.Bwana Amefufuka Haleluya

1. Bwana amefufuka,         Haleluya. Tuimbe na malaika, Haleluya. Sifa zetu na shangwe, Haleluya. Na zao zisitengwe. Haleluya. 2. Ukombozi timamu, Haleluya. Umetimu kwa damu Haleluya. Mshindi asifiwe, Haleluya. Yu hai kwa milele, Haleluya. 3. Jiwe, lindo, muhuri, Haleluya. Vi wapi? Na kaburi? Haleluya. Kifo hakimuwezi, Haleluya. Ametoka kuzimu, Haleluya. 4. Yu hai mtukufu, Haleluya. Cha kifo hatuhofu! Haleluya. Alitufia sisi, Haleluya. Tuwe huru na sisi, Haleluya. 5. Kichwa chatuangalia, Haleluya. Tupate nasi pia! Haleluya. Kwa kuwa tuna fungu, Haleluya. Mti, kaburi, mbingu, Haleuya. 6. Ndiwe Mwokozi wetu, Haleluya. Sifa ni yako Yesu, Haleluya. Utukuzwe pekee, Haleluya. Ni wewe ufufuo, Haleluya.  

118.Mle Kaburini Yesu Mwokozi.

1. Mle kaburini, Yesu Mwokozi! Alilazwa chini, Bwana  wangu!   Bwana! Amefufuka,    kifo kimeshindwa    kabisa! Gizani mle alitoka chini,  sasa atawala huko   mbinguni! Yu hai! Yu hai! Bwana Yesu yu hai. 2. Aungoja huo, Yesu Mwokozi! Mchana ujao, Bwana  wangu! Bwana! Amefufuka,…. 3. Walinda kaburi, Yesu Mwokozi! Bure ni muhuri, Bwana  wangu! Bwana! Amefufuka,…. 4. Kifo kimeshindwa,    Yesu mwokozi! Pingu zimevunjwa, Bwana Wangu! Bwana! Amefufuka,…

117.Yesu Amefufuka (Haya Shangilia)

1. K: Yesu    W:Amefufuka K:Yesu W:Amefufuka    ametoka kaburini K:/: Haya, W:Shangilia, K:Haya W:Shangilia, ametoka kaburini:/ 2. K:Shetani W:Ameshindwa, K:Shetani  W: Ameshindwa hana lake       duniani. K:/: Haya, W:Shangilia K:Haya W:Shangilia,   ametoka kaburini.:/ 3. K: Yesu W: Kawatokea, K:Yesu W:kawatokea wanafunzi       wake wote K:/: Haya, W:Shangilia, K:Haya Shangilia,      ametoka kaburini.:/ 4. K:Amani W:Iwe kwenu, K:Amani W:Iwe kwenu, mpokee       Roho wangu. K:/:Haya, W:Shangilia,      ametoka kaburini.:/ 5. K:Bwana   W:Yesu kapaa, sasa yu juu         Mbinguni K:/:Haya, W:Shangilia, K:Haya W:Shangilia,        sasa yu juu mbinguni:/ 6. K:Sasa W:Kristo huketi, K:Sasa W:Kristo huketi kuumeni       mwake Baba K:/:Haya, W:Shangilia, K:Haya W:Shangilia,        sasa yu juu ...

116.Amefufuka Kweli

1. K: Amefufuka    W: Kweli Yesu amefufuka           kutoka wafu K:Kaburini tupu. W:staajabuni nyote juu ya mwujiza huu K:Bwana Yesu W;Hayupo kaburini K:Yu hai W:Yu mzima daima K:Yeye ndiye W:Pekeee kashinda kifo. 2. K: Sisi Wakristo     W:Tunafurahia kwa shangwe           kubwa siku ya leo, K:Sababu Kristo W:Ameshinda Mfalme       mkuu wa dunia hii. K:Yeye ndiye W:Shetani mbaya sana K:Anapenda W:Kuwadanganya       Wakristo K:Waiachie W:Njia yenye uzima. 3. K:Sasa wenzangu W:Twende sote tumtumikie      Mfalme wetu. K:Tuwatafute W:Watu wengi wanaopotea maovuni. K:Tuwalete W:Kwake yesu Mwokozi K:Washiriki W:nasi furaha hii K:Haleluya, W:Kristo amefufuka. 4. K: Mungu apenda W:Watu wote wafike       Kwake        kwa kumwamini  K:wakamwimbie W: Kwa shukrani, Kwani wameshinda vita. K:Tumuombe W:Yesu asa...

115.Yesu, Yesu Amefufuka

1. K:Yesu, Yesu W:amefufuka. K:Yesu, Yesu W:amefufuka      Ameshinda dhambi na       mauti, amefufuka. 1. K: Akina Baba tumwendee W:amefufuka. K:Akina mama tumwendee  W:amefufuka K:Na sisi sote tumwendee W:amefufuka. K:Yesu, Yesu,… 2. K:Ujifunue na kwetu, W: Mwokozi wetu K:Utupe wokovu wako W: Mwokozi wetu K:Twakuamini, ee Bwana WMwokozi wetu K:Yesu, Yesu, W:Amefufuka      Ushindaji wako  huokoa Yesu Mwokozi. 3. K;Twakungojea kwa       shangwe, W:Yesu Mfalme K:Fahari yako tuone, W:Yesu Mfalme K:Na tukusifu daima, W:Yesu Mfalme K:Yesu, Yesu, W: Umefufuka       Sisi sote utatufufua        Siku ya mwisho.  

114.Amefufuka Katika Wafu

1. K: Amefufuka katika wafu,          akiwa na utukufu.          Kristo pekee,           ndiye mwenye nguvu. W:/:Yeye limbuko          la waliolala,           tena ni mwisho          wa nguvu ya mauti           kwetu.:/ 2. K: Hii ni habari iliyo kweli,           iletayo udhahiri          Yapasa wote,           tuache mashaka.     W:/: Yesu usifiwe,              Wewe pekee ndiwe              ustahiliye kushika               mamlaka yote:/ 3. K:Kristo u Bwana        mwenye uweza        Shetani ummeshinda,         kazi yote umeimaliza. W:...

113.Bwana Yesu Kafufuka

1. K: Bwana Yesu kafufuka,  ametoka kaburini. W: Haleluya, Haleluya,  ametoka kaburini 2. K. Na mashaka yalizuka,  hapakuwa tumaini, W:Haleluya, Haleluya, ametoka Kaburini 3. K: Wanawake walifika     asubuhi kaburini.   W:Haleluya, Haleluya,   ametoka Kaburini 4. K: Tayarini waliweka       manukato mkononi. W: Haleluya, Haleluya,       ametoka Kaburini 5. K: Walitaka kuupaka      mwili mle kaburini W:Haleluya, Haleluya,     ametoka Kaburini 6. K: Nao hao walifika;         Kumbe jiwe li kandoni.   W: Haleluya, Haleluya,           ametoka kaburini 7. K: Kwa ukweli malaika        kasimama kaburini. W: Haleluya, Haleluya,        ametoka kaburini. 8. K: Wakasema kafufuka;         enyi nyote kumbukeni. W:Haleluya, Haleluya,       ametoka kaburini...

112.Leo Siku ya Furaha

1. Leo siku ya furaha,     Kila mtu ashangilie,     Kristo Yesu afufuka,      ateka adui wote!     Haleluya! 2. Nyoka wa kale na kifo, Kuzimu hata ubaya Vimeshindwa  na mshindaji Yesu Kristo Mfalme  wetu! Haleluya! 3. Mateka yote ya kifo  yamekamatwa na Yesu,  na ufu umenyang’anywa  naye aliyefufuka! Haleluya! 4. Adui hawatushiki  tunakwenda uzimani,  tunapokunywa naye  kinywaji kipya milele! Haleluya! 5. Jua na mwezi na nchi, Viumbe vyote vya Mungu Vinafurahiwa leo: Mfalme wa uongo  ashindwa! Haleluya! 6. Kwa hivi tushangilie,  tumwimbie Yesu Kristo, Yeye ametuokoa,  afufuka kaburini! Haleluya!  

111.Siku Ya Furaha (Yesu Kristo Afufuka)

1. Siku ya furaha,    siku ya uzima   Yesu Kristo afufuka!   /:Watu kifungoni,   wamefunguliwa,  Furahini, furahini  Wakristo!:/ 2. Siku ya furaha,  siku ya uzima, Yesu Kristo afufuka! /:Kufa kumeshindwa,   uzima tayari! Furahini, furahini Wakristo!:/ 3. Siku ya furaha, Siku ya uzima, Yesu Kristo afufuka! /:Nguvu twapokea, Kumfuata sasa. Furahini, furahini Wakristo!:/  

110.Haleluya, Haleluya

1. Haleluya, Haleluya, Sauti na mioyo juu,  tumwimbie Mungu  nyimbo,  tumsifu na furaha, Aliyemwaga damuye  kwa ulimwengu wote,  amefufuka kifoni Sasa Yesu Mwokozi.  2. Minyororo yake kifo  imekatikatika pia,  na katika wafu wote Yee mzaliwa wa kwanza Yesu ameshinda sasa,   nasi twashinda naye. Ametupatia nasi  uzima wa milele. 3. Kristo afufuka kwanza     nao wengi baadaye.   Atakapokuja tena,     watatokea naye,     mavuno yatakuwako     mwisho wa ulimwengu,     watafika furahani      wote watakatifu. 4. Mwokozi amefufuka,  nasi tutafufuka. Tunyeshee kama mvua  neema yako ee Bwana. Tutafute yaliyo juu,  siyo ya ulimwengu,  na uzima tutapewa  naye Kristo kwa Mungu. 5. Tumsifuni, tumsifuni Mungu wetu, apaswa. Tumsifuni na Mwokozi,  aliyeshinda vita. Tumsifuni naye Roho,  kisima cha mapenzi.  Tumsifu...

109.Tumsifuni Mungu Enzini

1. Tumsifu Mungu enzini  na Mwana wake wa  pekee,  aliyefanya wokovu:  Haleluya! Haleluya! Haleluya! 2. Siku ya tatu mapema,  jiwe halijaondolewa,  akafufuka mshindaji. Haleluya! Haleluya! Haleluya! 3. Ametoka kuzimuni,  makosa hata shida zote,  zimetoweka kabisa. Haleluya! Haleluya! Haleluya! 4. Umemwumbua Shetani,  ukamvua mapambo yake,  ukafungua kifungo. Haleluya! Haleluya! Haleluya!  

108.Tumfurahie Daima

1. Tumfurahie daima, Yesu aliyefufuka Haleluya! Haleluya! Giza haliwezi kukaa, Jua limelifukuza.    Haleluya! Haleluya!    Haleluya! Haleluya!    Haleluya! 2. Naona Moyo wa Maria, Unashangalia sana, Haleluya! Haleluya! Nayo mioyo yetu sisi, Inapiga shangwe nyingi! Haleluya!..... 3. Jeraha zake za kufa, Zatupatia uzima, Haleluya! Haleluya! Na sasa anatawala Katika enzi ya Baba.   Haleluya!... 4. Mwokozi hakuogopa, Kuvuka maji ya kufa. Haleluya! Haleluya! Atupa nasi moyo mkuu. Tuongoze tufikee juu! Haleluya!....  

107.Kumekucha ni Mzima

1. Kumekucha, ni mzima Yesu aliyefufuka. Kaburi lake wazi, Kufa hakumshiki Yesu. Sina woga na kifo, Yesu amefufuka. 2. Kumekucha, ni mzima    Yesu, aliyefufuka!   Tunaitwa nduguze,     sababu anatupenda.   Tusiachane naye,    Yeye aliyeshinda. 3. Kumekucha, ni mzima Yesu aliyefufuka. Kamaba zitufungazo Zimekwisha funguliwa Mwili wangu uoze,  sina woga na kufa!  

106.Ameshsfufuka Kristo Kaburini

1. Ameshafufuka    Kristo kaburini,   Kwa hiyo twafurahia,   Tunapata upozi.   Uturehemu! 2. Asinefufuka   sote tungepotea,  alivyotoka kufani,   sisi tunamtumaini    Uturehemu! 3. Tumsifu Bwana!    Tumsifu Bwana!    Kwa hiyo twafurahiwa.    Yesu ni mtulizaji!    Uturehemu!  

105.Leo Shangwe Zitolewe

1. Leo shangwe zitolewe     shujaa atoka kufani.    Mtumishi wa Bwana huyu      aone kushinda kwake  /:Shangwe, shangwe    zitolewe!   Imbeni Haleluya!:/ 2. Mwana Kondoo amekuwa      leo simba mwenye nguvu.     Jiwe kubwa halimwezi,      kaburi lamfungukia.     Shangwe, shangwe….. 3. Bwana Yesu Umeshinda,    utupe uliyoteka:   Utengamanao wa Mungu    uliopata vitani!    Shangwe, shangwe…. 4. Yesu tunakutukuza,  twataka utugombee. Tuweza kushinda nawe, Kwa kuwa sisi tu wako. Shangwe, shangwe….

104.Yesu Amefufuka

1. Yesu Amefufuka,  sitakuogopa kufa. Amefufuka, naye  atanifufua mimi. Atanipa mwili mpya:  ni tumaini langu. 2. Yesu amefufuka,  anapatawala pote.    Nami nitatawala    pamoja naye milele.   Atimiza agano:   ni tumaini langu. 3. Yesu amefufuka,  yanipasa kumngojea. Mwenye kumtegemea Bwana wetu, ataona  rehema yake Mungu: Ni tumaini langu. 4. Yesu amefufuka,  naweza kumtumikia,  na shindana na tama,  moyo wangu uwe safi Atanisaidia: Ni tumaini langu. 5. Yesu amefufuka,  siwezi kutengwa tena  na Yesu Bwana wangu. Kwa mateso au furaha. Vyote havinishindi: Ni tumaini langu! 6. Yesu amefufuka,  ni mlango wa kuingia  furahani mbinguni. Nitatulizwa nikifa,  nikiweza kusema: U tumaini langu!  

103.Moyo Yafurahie Yafanywayo

1. Moyo yafurahie,      yafanywayo leo:    Mwanga umetokea  gizani mwa kufa. Mwokozi kalazwa,  tutakapozikwa,  roho ikiisha  kurudi mbinguni. 2. Alipozikwa Yeye  adui acheka. Lakini akashindwa: Kristo afufuka. Atokea shujaa  bendera mkononi,  kwani ameteka  mateka ya mwovu. 3. Ni jambo kubwa     hili lenye furaha kuu. Sitaogopa sasa  uchungu wa kufa,   na yote mengine   yatakayoteka    mali nipewayo   na Yesu Mwokozi. 4. Namshika siku zote Mwokozi wangu mkuu. Yeye ni kichwa chetu  sisi tu viungo. Dunia makosa Shetani na kufa Yeye kawashinda,  nami namfuata. 5. Afika furahani  nami nitafika, Sitaona huzuni Na shida zozote. Mkubwa wangu Yesu  ataniakingia  vinavyonidhuru, Yeye ngao yangu. 6. Nitakapoingia  mbinguni, naona  andiko la furaha Linasomwa hivi: Ashindaye kule Aingia hapa,  anayejidhili  atakuzwa hapa! ...

102.Haleluya Tumwimbie

1. Haleluya! Tumwimbie     tumsifu sana Bwana wetu,    tumshangalie kwa shangwe,   akafungwa na adui    alipokufa msalabani,   lakini sas yu hai.   Habari njema hii:   Mesiya anakaa mzima kweli.   Haleluya! Tumsifuni!   Tumsifuni Mungu wetu. 2. Haleluya! Tumwimbie,  tumsifu sana Bwana wetu,  tumshangilie kwa shangwe Watu wana shida sana,  taabu nyingi na huzuni  mpaka watakapokufa. Furaha yetu hii: Bwana ametoka kaburini. Haleluya! Tumsifuni! Tumsifuni Mungu wetu! 3. Haleluya! Tumwimbie  tumsifu sana Bwana wetu,  tumshangilie kwa  shangwe. Atatufufua sisi,  tutafika rahani kwake,  tuishi pamoja naye. Tumwamini Yeye  Mwokozi wetu mkuu,  mwenye nguvu. Haleluya! Tumsifuni! Tumsifuni Mungu wetu!  

101.Moyo Wangu Amka Hima

1. Moyo wangu amka hima,    Jua limetokea.    Ondoka usingizini,     mpokee mponya wako,     atokaye kaburini,     kashinda nguvu za kifo     watu wafurahishwe. 2. Fufuka pamoja naye,  uyaache mabaya! Maliza mwenendo wako  ukimngojea Yesu,  aliyekwenda mbinguni. Kwa hiyo nawe ufanye  yampendezayo yeye. 3. Ukiwa na wasiwasi Yesu anauweza: Ukipatwa na huzuni, Yeye furaha yako. Umtwike Bwana mzigo. Usisumbuke: yu hapa,  kwani amefufuka. 4. Usimwogope shetani,  kifo hata kuzimu Shida za kufa nyepesi Mwokozi Yesu ni mzima. Shuja wetu haondoki,  awagombea wanyonge  wanaomtumaini.  

100.Mungu Tusaidie

1. Mungu tusaidie,     sisi tunaangamia.     Nchi imeharibiwa      na mwovu wake Shetani    Kweli kweli ndiye Yesu     aliyewambwa mtini      penye mlima wa     Golgotha      aokoe wenye dhambi. 2. Kaonyesha huruma,   Wayuda wakasumbua.   Wakampiga makofi,   Pilato aliamua.       Kweli kweli ndiye Yesu… 3. Yesu mwenye upendo    alikubali kuuawa,     damu ilimwagika     ili sisi tuokoke.         Kweli kweli ndiye Yesu….. 4. Pale msalabani, Bwana Yesu aliteswa  mzigo wa dhambi zetu,  ulimwangukia yeye,  Kweli kweli ndiye Yesu….. 5. Sote na tukumbuke,  kifo cha Mwokozi wetu. Alisema ya kwamba  jililieni wenyewe.     Kweli kweli ndiye Yesu. 6. Habari zilisemwa,     Mahali hapa hayupo,      ona alipokuwa,      jiwe limeon...

99.Yesu Alitufia

1. Yesu alitufia, tumshukuru! Tumshukuru Bwana  wetu, Tumshangilie Yesu Mwokozi. 2. Sisi watu wabaya,    tumshukuru!          Tumshukuru….. 3. Wakamvua mavazi,      tumshukuru!      Tumshukuru…. 4. Walimchezea Bwana,     tumshukuru!      Tumshukuru…. 5. Aliteswa Golgotha,    tumshukuru!    Tumshukuru… 6. Kasema imekwisha,    tumshukuru!       Tumshukuru…. 7. Hakushindwa na kifo,     tumshukuru!      Tumshukuru… 8. Katoka kaburini,     tumshukuru!     Tumshukuru… 9. Kafufuka kwa wafu,      tumshukuru!      Tumshukuru. 10. Ndiye Mwokozi wetu,        tumshukuru!        Tumshukuru…. 11. Ataishi milele,       tumshukuru!          Tumshukuru…  

98.Mungu ameona Tulivyo

1. K: Mungu ameona W: Tulivyo huku chini, K: Neno hilo jema W: Litokalo mbinguni    /: Ya kwamba Yesu kaja    na kutuongoza,    tufike uzimani.:/ 2. K: Hujui njia W: Uende upande gani K: Nuru yake Bwana W: Huangaza njiani.   /: Ya kwamba Yesu…. 3. K: Kweli, unajua, W: Mtu wa duniani. K: Atakuongoza W: Upate kuamini.    /: Ya kwamba Yesu…. 4. K: Njooni tufungue W: Milango ya moyoni K: Neno lake Bwana W: Likaingie ndani.   /: Ya kwamba Yesu…  

97.Mwana Kondoo wa Mungu Uichukuaye Dhambi

1. Mwanakondoo wa Mungu Uichukuaye dhambi yote, Mwana Kondoo wa  Mungu, Uturehemu wakosaji, Mwana Kondoo wa Mungu. 2. Mwana Kondoo wa Mungu Uichukuaye dhambi yote, Mwana Kondoo wa Mungu, Utuhurenemu wakosaji, Mwana kondoo wa  Mungu. 3. Mwana Kondoo wa,     Mungu    Uichukuaye dhambi yote,   Mwana Kondoo wa     Mungu,    Utupe amani yako,    Mwana Kondoo wa      Mungu.Amen   

96.Wakristo Twabeba Nini?

1. K: Wakristo twabeba nini? W: Msalaba wake Yesu;     Twenda    twashutumiwa. 2. K: Wakristo twavaa nini? W: Twavaa vazi la Yesu; Twaenda twashutumiwa. 3. K: Wakristo twaenda   wapi? W: Twaenda njia ya Yesu, Ni njia yenye mateso. 4. K: Mwokozi twamwona    pale, W: Ateswapo Goligota; Kwa uchungu anapita 5. K: Wakristo tuvumilie W: Njia hii yenye shida. Mwisho wake tatashinda. 6. K: Tushinde kwa nguvu    gani? W: Yesu ni ushindi wetu. Katoa ahadi kwetu. 7. K: Mwokozi wetu    kashinda W: Mauti nalo kaburi. Yu hai hata milele.  

95.Bwana Yesu Alikufa

1. Bwana Yesu alikufa  kwa sababu yetu sisi,  alipata duniani  maumivu mengi sana. 2. Bustanini akiomba  akafadhaika kabisa.  Jasho lake kama damu  nchini ikadondoka. 3. Wayuda wakamwendea,  wakamshika,  wakamfunga.  Na rafiki zake wote  wakimbia, wakamwacha. 4. Na wale wakampeleka  barazani kumhukumu.  Wamhukumu yule  mfalme,  atakayewahukumu. 5. Wakamfyoza, wakampiga,  wakampeleka Golgota.  Pale wakamwamba mtini,  kwa misumari kumkaza. 6. Kukawa na giza huko,  nchi ikatetemeka.  Watu walioko wote,  Wakaona woga mwingi. 7. Na saa tisa ikifika,  Yesu apaza sauti kuu,  kwamba: Yamemalizika;  mara akakata roho. 8. Askari wakamwendea,  wakamwona amekufa.  Nao wakamchoma mkuki;  ukapenya moyo wake. 9. Damu yake ikatoka,  yakatoka maji tena.  Maji, damu iwezayo  kuosha uchafu wote. 10. Na watu wema  wamshusha,  wamfunga katika sanda, ...

94.Unipe Nguvu Bwana

1. Unipe nguvu,  Bwana nikumbuke  mateso yako yaliyokupata,  kutukomboa tulioanguka  katika dhambi. 2. Umemtii Baba,  mpaka kufa kwako  mahali petu ulisulubishwa,  makosa yetu yalikua  mengi, umetufia 3. Wokovu wangu  ulinitafuta; nakuangukia  Mwokozi wangu,  nakushukuru nikiitazama  huruma yako.  

93.Njoo Msalabani

1. Njoo msalabani  ukilemewa,  wewe msafiri!  Kwenye msalaba  utapumzika,  ndiyo raha. 2. Wamwona Mwana  Kondoo wa Mungu,  akichukua   mshahara mkuu  wa makosa yako  akufia 3. Yesu asiye mkosaji hata,  ahukumiwa.  Waona jinsi akupendavyo  awe mdhambi?  

92.Ukiwa na Vichache

1. Ukiwa na vichache Umtolee Bwana,  kwani akiba yako  ataiongeza.  Vipaji vyako haba. Yeye hakatai, kidogo kwako wewe, kwake kitazidi! 2. Vile vile na moyo  umtolee Bwana! Ndivyo vipaji vyema  vinavyompendeza. Kwani sisi wenyewe,  alitukomboa,  akiuawa Yeye  kwa kuwambwa mtini. 3. Ukiwa na ubaya  umwambie Bwana! Ukishandana nao,  atakutakasa. Damu aliyotoa,  ndiyo itoshayo,  kuosha wakosaji,  hata wewe hivyo. 4. Vitu vya mali nyingi  umtolee Bwana!  Alitoka mbinguni  kusumbuka hapa.  Alikufa mwenyewe  kwa ajili yako,  nawe hutoi chako  kwa ajili yake? 5. Wakristo na tutoe      shukrani kwa Mungu.      Hiyo ndiyo shukrani       ya wokovu wetu.     Injili yake Kristo,       ienee pote!         Kwa ushuhuda wetu        watu waokoke.  

91.Ni damu Idondokayo

1. Ni damu idondokayo  mwilini mwa Yesu,  wakosaji wakioga,  husafishwa kweli    Bwana wangu.  Mungu wangu,  U uzima wangu,   umekutana na kufa   kwa ajili yangu! 2. Ilimpatia wokovu  mwizi kule mtini,  nami nisiyemtafuta,  inanisafisha.  Bwana wangu…. 3. Shaushi aliyemlinda Yesu akiteswa,  naye akamshuhudia:  ni mwana wa Mungu! Bwana wangu…. 4. Nipe ulimi mpya Yesu     wa kukuimbia,    Babayo tutamtukuza  Jina lake pekee.    Bwana wangu…..   

90.Mtini Mponya Alipowambwa

1. Mtini Mponya alipowambwa,  ndipo nimwombapo upozi  akaniokoa mpenzi.  Mwana wa Mungu.    Mwana wa Mungu    Mwokozi wangu.    Mtini mponya     alipowambwa,    Mwana wa Mungu! 2. Chini ya mti wenye     uchungu,    ndipo nimwombapo usafi,    mara kwa damu kaniosha    Mwana wa Mungu.      Mwana wa Mungu…. 3. Akaniondolea manza,  ameingia ndani mwangu,  kwani mtini amenifia. Mwana wa Mungu. Mwana wa Mungu…. 4. Ziwa la damu ya kiasi,      linatosa makosa yote,     laniendesha wokovuni.    Mwana wa Mungu.    Mwana wa Mungu….. 5. Hicho kijito chenye mali! U tayari kuzama humo? Humo utaona uzima! Mwana wa Mungu.    Mwana wa Mungu…..  

89.Kumbuka Getsemane

1. Kumbuka Getsemane,    asongapo shetani, Mwokozi ukamwone  ateswavyo shambani;  nao uchungu wewe,  aombapo kumbuka! 2. Kumbuka barazani     ashtakiwapo Yesu:     mtazame Bwana Huko,    walipomuhukumia     upate soni wewe,    mti wa Yesu kumbuka! 3. Kmbuka na Golgota    alipokufa Bwana.   Upaji wa tambiko    ameutoa Yeye.   Kasema: Imekwisha   Mti wa Yesu kumbuka! 4. Kumbuka bustanini     walipomzika Yesu,     kukiwa bado giza.     Mfu amekwenda wapi?    Amefufuka Yeye;    Ufufuko kumbuka!  

88.Nataka kusimama

1. Nataka kusimama  chini ya msalaba,  kama kivuli cha mwamba wakati wa mchana,  kama ni maji nyikani,  kambi safarini,  na hapa nitapumzika,  kwani jua kali. 2. Mahali pema sana  chini ya msalaba,  kwani hapo ninaona  upendo wa Yesu. Yakobo alivyoona  ndotoni zamani,  mti Yesu aliowambwa,  ni ngazi kwa Mungu. 3. Juu ya msalaba huo Yesu alikufa Alikufa tuokoke. Tuliopotea. Ninastaajabu kabisa  ni mambo mawili: Kwake Yesu ni upendo, Kwangu mimi kosa! 4. Wataka kuonana  na Yesu mbinguni, y akupasa kukaa kwanza  chini ya mti huo. Ni kweli siku chache tu  mateso na shaka. Halafu pasipo mwisho  furaha kwa Bwana!   

87.Ee, Watoto Njooni

1. Ee, watoto njooni,  njooni Golgota,  mtazameni Yesu  aumizwavyo! 2. Mtazameni huko Mkamtazame, Sogeeni kwake,  ametupenda. 3. Sogeeni kwake,     mkamtazame,    mioyo iyeyuke,   mwangukieni! 4. Mioyo imililie Anayeteswa,  mzigo wetu mkubwa  aukubali. 5. Mzigo wa makosa    ya ulimwengu.   Mpeni nanyi nyote    mioyo yenu! 6. Apata mshahara, Ni kufa kwake, Wewe una raha, Kwake ni kufa 7. Atoa enzi     ya utukufu.   Tuimbe Haleluya    na kumshukuru.  

86.Roho Yangu Tua Hapa

1. Roho yangu tua hapa Mlimani pa Golgota, Angalia tendo hili, afanyalo Mfalme mkuu. Amevutwa na upendo kuacha enzi yake. 2. Yesu alivyotupenda,  twaona msalabani,  maumivu hata manza ya makosa yampata. Anakaa mahali petu, Sikia ateswavyo! 3. Kufa kwako kunivute nife pamoja nawe Mwili na mapenzi yangu,  yazikwe nawe Bwana. Niwe na kutengemana,  mwenye pendo la kweli!  

85.Uliyesulibishwa

1. Uliyesulubishwa, Mtakatifu Bwanangu, Uwe ngao shidani,   uniombee mimi. Uliyesulubishwa, Mtakatifu Bwanangu! 2. Wongofu sina hata,  niondolee makosa.  Mwovu akinishtaki  nasumbuka rohoni. Wongofu sina hata,  niondolee makosa. 3. Wewe tu nipokee,     nakukumbilia wee.     Hata nifanye bidii,    nikatoe machozi.   Wewe tu nipokee,   nakukimbilia wewe 4. Uwe ngao shidani, Niombee na mimi! Hapa nikiumizwa, Saa ya mwisho ikija: Uwe ngao shidani, Niombee na mimi!  

84.Nimshangilie Bwana Wangu

1. Nimshangilie  Bwana wangu  na kumwimbia Mkombozi, katukomboa msalabani, nisifu pendo lake kuu.     Haya mwimbieni Yesu,     amekubali mateso     katukomboa     msalabani,     tusifu pendo lake kuu! 2. Tumsifu Yeye  Mponya wetu  katika ulimwengu huu,  katupatanisha na Baba tulio wakosaji tu.       Haya mwimbieni... 3. Katuletea mwanga wake,     tulikaa katika giza,     wokovu ukaonekana,    kamshinda mwovu,    ni shujaa!        Haya mwimbieni…. 4. Na tumtukuze Bwana      wetu,     tumtumikie kwa bidii,    na atawale apendavyo,     na sisi sote tuta mtii!     Haya mwimbieni……  

83.Yesu Kuteswa Kwako

1. Yesu kuteswa kwako  nitakufikiri. Nipe kwa shauri hili roho na mbaraka. Moyo wangu uone  hali yako Yesu, jinsi ulivyoteswa  kwaajili yetu. 2. Moyo wangu uone  taabu yako kubwa,  maumivu, mapigo,  na kuwambwa mtini,  taji lako la miiba  tena misumari,  iliyokuumiza,  hata kufa kwako. 3. Nikitazama yote  yaliyokutesa,  nikifikiri sababu  na maana yake. Sababu ndio mimi  na makosa yangu:  umepata mateso,  nipate huruma. 4. Yesu unifundishe  nijute kwa moyo;    nisikuzidishie  shida na uchungu. Nisiweze kupenda  yaliyokutesa: nataka kuyaacha  na kukufuata.

82.Mwana Kondoo wa Mungu Unachinjwa

1. Mwana kondoo wa Mungu  unachinjwa msalabani  wavumilia sana  ujapodharauliwa. Waichukua dhambi,  tupate kuokoka. Utuhurumie ee Yesu. 2. Mwana kondoo wa Mungu  unachinjwa msalabani  wavumilia sana  ujapodharauliwa. Waichukua dhambi,  tupate kuokoka.  Utuhurumie ee Yesu. 3. Mwana Kondoo wa Mungu  unachinjwa msalabani  wavumilia sana  ujapodharauliwa. Waichukua dhambi,  tupate kuokoka.  Tutulize mioyo ee Yesu.  

81.Ulimwengu tazama

1. Ulimwengu Tazama, Yesu mwokozi wako   asulubiwavyo. Mwenye heshima Yote  anayavumilia  mateso tena matusi. 2. Karibia tazma     maungo yake yote     yatokavyo damu.    Na moyo wake mwema    kwa shida na uchungu     unaugua vigumu. 3. Nani akupigaye,    aliyekufanyia    mambo kama haya?   Wewe huna makosa    kama wengine wote,    hujui kosa lolote. 4. Makosa yangu mimi yaliyo kama mchanga, hayahesabiki, ndiyo yakutiayo  mateso na chungu  uliyoyavumilia. 5. Mimi nimestahili  kulipa haya yote, na kufungwa sana. Mapigo na mateso uliyoyapata wewe yalitoka kwangu mimi. 6. Umejitwika mzigo  ulio mzito sana  kuliko jiwe kuu. Wachukua maovu, Tupate kuokoka tukae nawe daima!

80.Liko Neno Moja Nipendalo

1. Liko Neno moja nipendalo, ni chakula cha moyo, Neno hili linanituliza  nikipatwa na shida: Kumtazama Bwana Wetu  pale,  atoapo jasho kama damu, akubalipo mzigo, Baba aliomtwika 2. Siku zote  namkumbuka yeye,  alivyosulubishwa,  akivumilia taabu kimya  kama mwana wa kondoo. Nami akanikumbuka  mimi, akisema: Yamemalizika! Huko aliniteka,  nami niwe mtu wake. 3. Bwana wangu,  u mwenye huruma,  mimi ni mkosaji tu;  nilipokuwapo penye giza  wewe ukatokea,  ukamtafuta kondoo wako,  kabla mimi sijakusikia. Watoa ukombozi  unipao uhuru. 4. Ndimi huru lako, Bwana Yesu,  wewe ndiwe Bwanaangu. Jina lako, bora liung’aze moyo wangu vizuri. Amani yako nikae nayo, Siku zangu zote mpaka  kufa. Ndivyo ninavyoomba, Bwana unikubali.  

79.Nakusalimu Kichwa

1. Nakusalimu kichwa Kilichojaa damu, Kilichovikwa taji La miiba mikubwa, Kilichopata enzi Kwa Mungu mbinguni, Kitukanwacho sasa Matusi makali. 2. Naona uso wako  watemewa mate,  heshima yako yote  imeondolewa. Mwanga wa macho yako wazimika sasa. Aliyekuharibu   hivi, ndiye nani? 3. Mateso yako Bwana, Yanipasa mimi. Wewe waadhibishwa Kwaajili yangu. Hukumu unapata Iliyonipasa. Bwanangu nakuomba, Unihurumie! 4. Na mimi na simama  msalabani pako; niwe karibu kwako utoapo roho; ukiugua sana  kwa teso la kufa,  nitakushika Bwana kwa moyo wa upendo. 5. Bwana nayashukuru  masumbuko yako,  sababu ya kuteswa  na kufa kuchungu. Wewe umenishika,  nami nakushika,  mwisho nitakufia  uliyenifia. 6. Moyo unaposhikwa  na woga wa kufa,  usiniache Bwana  katika vita hii. Siku ya kufa kwangu  unisaidie,  kufa kwako kuchungu  kutaniokoa. 7. Niwie kama ngao  nitakapokufa,  nione uso wako katika u...

78.Mwokozi Wangu Umekosa Nini?

1. Mwokozi wangu  umekosa nini?  Wahukumiwa kama mwuaji. Umeshtakiwa makosa Mangapi uliyotenda? 2. wapigwa sana   miiba taji lako, umetemewa  mate, watukanwa,  wanyweshwa nyongo  tena siki kali. 3. Sababu gani  unateswa hivi? Makosa yangu yanakuumiza;  mateso haya yako yanipasa,  mimi mkosaji. 4. Ajabu kubwa  sana tendo lako; mchungaji unateswa kwa ajili ya kondoo, Bwana  unawalipia watumwa wako. 5. Tuliopokuwa mateka wa mwovu,  nawe ukaja ukatukomboa. Tulistahili kufa kwa Milele, Ukatufia. 6. Mwokozi wangu  nifanyaje mimi,  niitangaze pote sifa yako? Nakufuata nikutumikie  maisha yote.  

77.Mwana Kondoo wa Mungu Waiondoa Dhambi

1. Mwana kondoo wa Mungu  waiondoa dhambi; Tuhurumie. 2. Mwana Kondoo wa Mungu waiondoa dhambi; Tuhurumie. 3. Mwana Kondoo wa Mungu Waiondoa dhambi; Ututulize.Amen.  

76.Mwana Kondoo Ayalipa.

1. Mwana Kondoo ayalipa Madeni ya dunia. Ayachukua makosa Ya wakosaji wote. Aenda na kuugua, Anakubali kuchinjwa, Furaha aziacha. Wanamhukumu wampiga, Wanamtukana wamtesa, Asema: Nakubali 2. Mwana Kondoo ni Mwokozi Ni mponya wa mioyo; Aliyetumwa na Mungu Awakomboe watu. Mwanangu, nenda okoa Watoto niliotupa Sababu ya makosa. Dhambi zao ni nyingi Mno; Watolee ukombozi Damu na mwili wako. 3. "Tayari mimi, Babaangu, Nitwishe nichukue. Maneno uyasemayo Nitafuata yote". Pendo hili kubwa sana,  lamshika Baba wa mbingu  amtoe mwana wake. Pendo hili lina nguvu, Linamlaza kaburini Aletaye uzima. 4. Sitasahau pendo hili Bwanangu siku zote, Nitakushika daima, Kama unishikavyo. Mwanga wa roho ni wewe; Roho inapozimia Niwie moyo wangu. Na tuagane, Bwanangu, Niwe mali yako sasa Na halafu mbinguni.

75.Mikononi mwa Mitume

1. Mikononi mw a Mitume Kazi ilifanywa, si nguvu Yao Walipewa msaada, ndiye Roho. Wakapata kuona upya tena.     /:Nenda,(kazini tu)        nenda, (siache)  kuyasema.:/ sisi ni badala yao. Mitume wa zamani Tupe vipawa vya kazi, /:tuifanye(tuifanye) Kazi yako (kazi yako):/ Ututume, ututume, Ututume. 2. Tuombe kupata Roho Tuende kazini. Si nguvu yetu kwa wafanya kazi hii njema mno. Tutakwenda haraka Kuifanya.   Nenda, nenda….. 3. Vuvia Roho Mtakata Ndani mioyoni utuhuishe Tupe moto wa Roho, Tusimame Tuwe tayari kwenda kutumika.  Nenda, nenda…  

74.Bwana Uliyewaita Watakatifu

1. Bwana uliyewaita, Watakatifu wako, Wawe mitume, wachunga, Walishe kundi lako, Wanyonge na wenye hofu Wakawa mashujaa, Na wapole wa kunena Wasiwe kunyamaa. 2. Hata leo wawataka Watakatifu wako, Nawe wauliza, Ni nani aliyeko Atakaye nimtume Afundishe vijana? Ni tayari, Bwana wangu, Nitume mimi Bwana. 3. Nitume na mimi, Bwana, Kama ulivyotumwa, Habari ya msamaha, Na dhambi kutubiwa, Niwahubiri wakosa, Na walopotea, Wokovu u wake Bwana, Aliyewafilia. 4. Astahiliye hapana Kutamka habari, Lakini Wewe waweza  kutufanya tayari neno lako tulijue, tupe na Roho wako, hayatakuwa ya bure, haya maneno yako.  

73.Ni Ujumbe wa Bwana

1. Ni ujumbe wa Bwana Haleluya! Wa maisha ya daima. Amenena mwenyewe, Haleluya! Utaishi ukitazama.       Tazama! Ishi sasa!        Kumtazama Yesu.        Amesma mwenyewe,        Haleluya!        Utaishi ukitazama. 2. Ni ujumbe wa wema, Haleluya! Nawe shika, rafiki yangu. Ni habari ya raha, Haleluya! Mwenye kuisema ni  Mungu.             Tazama… 3. Uzima wa daima, Haleluya! Kwake Yesu utauona. Ukimtazama tu, Haleluya! Wokovu pekee wa Bwana.      Tazama….

72.Tumesikia mbiu

1. Tumesikia mbiu: Yesu, loo! Aponya; itangazeni kote, Yesu loo! Aponya. Tiini amri hiyo: Nchini na baharini, enezeni mbiu hii: Yesu loo! Aponya. 2. Imbeni na vitani: Yesu loo! Aponya; Kwa nguvu ya Mkombozi, Yesu, loo! Aponya. Imbeni wenye shida, Unapoumwa moyo, Na kaburini imba: Yesu, loo! Aponya. 3. Mawibini ienee: Yesu, loo! Aponya: wenye dhambi jueni: Yesu, loo! Aponya Visiwa na viimbe, vilindi itikeni, nchi shangilieni: Yesu, loo! Aponya. 4. Upepo utangaze: Yesu, loo! Aponya; mataifa ya shangaa; Yesu, loo! Aponya. Milimani, bondeni, Sauti isikike ya wimbo wa washindi: Yesu, loo! Aponya.

71.Wajibu Mwema watoka Kwako

1. K: Wajibu mwema         watoka kwako        Bwana mwenye         utukufu.        Neno jema ndilo Jina        lako.   W: /: Yesu ni mwanzo       wa kazi shambani,       tena ni Bwana,       wa nguvu kwa utume         wetu.:/ 2. K: Watendakazi mwako          shambani,         uwape matumaini.         Nazo nguvu wakiwa           kazini. W: /: Watende yote kwa          uaminifu,          wawe makini,          huduma isiharibike.:/ 3. K: Wapate heri         kuyasikia uliyoyaagizia.         waje nao kutuhubiria. W:/: Tena kazini        wakaelezee Neno       kwa wazi, ...

70.Twende Vitani

1. Twende vitani vitakatifu, Zikitujia , shida na taabu. Ngurumo zivume kutia Woga.      Mwiteni Mwokozi!  Yesu mwanga. 2. Ingawa giza lawafunika, Na raha yenu ikizimika, Na nguvu za muovu  hazina mpaka     Mwiteni Mwokozi…. 3. shetani aje, akijaribu Kuvunja kazi na kuharibu Hila zake zote na  zitakwisha.     Mwiteni mwokozi

69.Wito Waja

1. Wito waja, kwa nchi zote   Wapi washindi wa Yesu   Watakaomfuata kweli?   Sisi tujitie kwake!   Mkubwa nani?   Tushikane   naye mfalme, tupatane,   tumfuate! 2. Ana ufalme tangu kale,    Nchi hata mbingu ni zake.    Atuelekeza juu kwake,    Hatahukumiwa tena.       Mkubwa nani?.... 3. Tutangaze utume mwema    Kwa makabila ya kwetu,    Na tuseme pasipo woga    Tuyaonayo kwa Yesu.         Mkubwa nani?... 4. Haya jamaa tuwe tayari    Sisi watumishi wake,    Yeye ni mfalme wa    majeshi,    Mili na mioyo ni yake.          Mkubwa nani?...  

68.Nitakutukuza

1. Nitakutukuza, Nakuimbia /: wewe uzima wangu, Kingojeo change!:/ 2. Umeniokoa kwa   mkono wako, /: nalifuta njia Ya upotevuni.:/ 3. Wote wakujue Upole wako, /:wakufuate Yesu Ninayekupenda.:/ 4. Utume mitume Waende kote, /:kwa nguvu yako Bwana Wafu wafufuke.:/ 5. Huku chini kote, dunia nzima /: lifanywe kundi moja, Wewe Mchunga wao!:/

67.Nyesha Mvua

1. Nyesha mvua, nyesha Mvua, Wewe Roho wa Baba, Nchi kavu ikanyweshwe, Imsifu Mungu wetu! 2. Vuma sana, vuma sana Roho mwenye uzima, Tulio na usingizi Utuamshe kwa mkono! 3. Toa mwanga, toa mwanga, Roho kwani unang”aa Wewe ushinde usiku Tusikae na giza. 4. Sikiliza, sikiliza,  wewe mfalme wa mbinguni!  Tuma Roho wako kwetu, Kote kuwe na upya!

66.Mfalme ni Yesu Pekee

1. Mfalme ni Yesu pekee, Wote wanamwangukia, Watawalishwa na Mungu, Ndimi zote ziungame Yesu ni Mfalme wa pekee, atukuzwe popote. 2. Mfalme mkubwa, Watu wako Wakutii, wanakusifu. Yesu apita wafalme, Yeye ndiye mkubwa sana, apenda kuwakomboa, kwani ndiye Mwokozi. 3. Enyi watu mpeni mioyo, Mnaohuzunika njooni; Wakiwa semeni naye, Kwani vyote aviweza. Awagawia uzima Wanaomngoja yeye. 4. Kama wataka uzima, nenda kwake, acha soni, Yeye anakungojea. Amejitoa mwenyewe, wewe upate kurithi, Mbingu ni yako sasa. 5. Nimsifuje Yesu Kristo Mimi vumbi, mimi jivu? Nasema: nitamtangaza Kristo Yesu ndiye Bwana! Na tumpende, Tumheshimu Sifa zote zampasa.  

65.Yesu ni Mponya

1. Yesu ni Mponya, Aleta furaha! Mwanzo na mwisho Wa vyote ndiye. Mwana Adamu Na Mungu wa kweli Ametujia atubariki. Mbingu, dunia, Toeni habari: Yesu ni Mponya, Aleta furaha! 2. Yesu ni Mponya, Aleta wokovu! Sikilizeni habari njema! Sisi tulipomwacha  Mungu wetu akaturudisha tena kwake. Ametufanya watoto wa Mungu Yesu ni   Mponya, aleta wokovu.. 3. Yesu ni mponya, Aleta uzima! Kamba za kufa zimekatika. Mwana wa Mungu Kumshinda shetani, Awakomboe watumwa wake, amewapata kawapa uhuru. Yesu ni mponya, aleta uzima. 4. Yesu ni Mponya, Mchungaji wa kweli, anayelisha vizuri kondoo. Wote walio mbali awaita, Awarudishe kundini mwake. Awakomboa kondoo kufani: Yesu ni Mponya Mchungaji wa kweli. 5. Yesu ni mponya na Mfalme wa enzi! Mbingu zimsifu na watu  wamtii. anageuza mioyo ya watu, hata na sisi tumpe yetu, kwani anapenda kutupa uzima. Yesu ni Mponya na mfalme wa enzi!  6. Yesu ni Mponya na mwenye upendo! Anatupenda kwa moyo wote. yeye mwenyewe upendo wa kweli, a...

64.Yesu Mwokozi

1. Yesu Mwokozi mwenye nguvu zote, wewe Mwana wa Mungu nitakupenda, nitakusifu, Uliyempenzi wangu mkuu . 2. Uzuri wote Wa nchi na milima Unatufurahisha. Yesu ni mzuri kupita hiyo anatufariji sisi. 3. Jua na mwezi Hata nyota zote zinang’aa mbinguni. Yesu ashinda uzuri huo, ang’aza watu mioyo. 4. Uzuri wote  hapa na mbinguni  ni mfano wa Mwokozi Tumpende Yeye wa  utukufu aliyetupenda kwanza.  

63.Yesu mfalme Utiishe

1. Yesu,mfalme,utiishe Upesi ulimwengu wote, Viumbe vyote vikutii. Ubariki neno lako, Utoe roho wa uzima, Uamshe wanaolala. Bwana, usikie Tunavyokuomba. Amen, Amen! Tutaimba Haleluya Na nyimbo za kusifu.  

62.Uamke Kwetu Tena Roho

1. Uamke kwetu tena Roho wa mashaidi wale wa  kwanza, waliokesha siku zote, waliomshinda yule adui, wakihubiri Neno la Yesu kwa watu wa ulimwengu wote. 2. Uwashe moto wa upendo, Uendelee pote kuwaka. Peleka watu mavunoni, Wanaofanya kazi kwa bidii. Bwana mwenye mavuno, Tazama: Watenda kazi yako ni haba. 3. Mwanao ametuagiza kuomba hivi kwa jina lake, na sisi wanafunzi wake, twashika neno lake kwa bidii. Twaomba hivi kwa moyo  wote. Ee Bwana usikie, ufanye! 4. Utume watu wengi sana, walitangaze Neno kwa nguvu. Tusaidie, tuokoe; Ufalme wa shetani uishe. Usimamishe, Bwana wa Mbingu, Ufalme wako Ulimwenguni! 5. Utume mwema na uende mahali popote huku nchini. Wa dini zote waingie kundini mwako mwa  wateule. Amsha nao Wana wa ahadi Na wa Imani zote wakutii.