105.Leo Shangwe Zitolewe
1. Leo shangwe zitolewe
shujaa atoka kufani.
Mtumishi wa Bwana huyu
aone kushinda kwake
/:Shangwe, shangwe
zitolewe!
Imbeni Haleluya!:/
2. Mwana Kondoo amekuwa
leo simba mwenye nguvu.
Jiwe kubwa halimwezi,
kaburi lamfungukia.
Shangwe, shangwe…..
3. Bwana Yesu Umeshinda,
utupe uliyoteka:
Utengamanao wa Mungu
uliopata vitani!
Shangwe, shangwe….
4. Yesu tunakutukuza,
twataka utugombee.
Tuweza kushinda nawe,
Kwa kuwa sisi tu wako.
Shangwe, shangwe….
Comments
Post a Comment