81.Ulimwengu tazama

1. Ulimwengu Tazama,
Yesu mwokozi wako  
asulubiwavyo.
Mwenye heshima Yote 
anayavumilia 
mateso tena matusi.


2. Karibia tazma 
   maungo yake yote 
   yatokavyo damu.
   Na moyo wake mwema
   kwa shida na uchungu 
   unaugua vigumu.


3. Nani akupigaye,
   aliyekufanyia 
  mambo kama haya?
  Wewe huna makosa 
  kama wengine wote, 
  hujui kosa lolote.


4. Makosa yangu mimi
yaliyo kama mchanga,
hayahesabiki, ndiyo yakutiayo 
mateso na chungu 
uliyoyavumilia.


5. Mimi nimestahili 
kulipa haya yote,
na kufungwa sana.
Mapigo na mateso
uliyoyapata wewe
yalitoka kwangu mimi.


6. Umejitwika mzigo 
ulio mzito sana 
kuliko jiwe kuu.
Wachukua maovu,
Tupate kuokoka
tukae nawe daima!




Comments

Popular posts from this blog

17. Tuimbe na kusifu

32 Kitoto Mpenzi Lala Wee

143.Mungu ni wa Utukufu