Posts

Showing posts from September, 2023

170.Yesu Wangu Simwachi

1. Yesu wangu simwachi,     kwani amenikomboa. Akitoa maisha,  kulipa madeni yangu. Sasa namwelekea,      Yesu wangu          simwachi! 2. Yesu wangu simwachi,  siku zote za duniani. Nimempa yangu yote,  ayashike mikononi.       Sasa namwelekea…. 3.Yesu wangu simwachi,      anichunga kwa upole    malishoni vizuri, mwenye shangwe  ampendaye: Sasa namwelekea…..  

168.Shika Mikono Yangu

1. Shika mikono Yangu,  niongoze,  mpaka nimalizapo  safari hii. Nikiwa peke yangu  napotea. Po pote uendapo  nipeleke! 2. Tuliza moyo wangu,  uwe kimya,  nikiona furaha au  majonzi,  unitulize sana,  ndimi wako,  sitaki neno tena, ila hilo. 3. Nisipoona leo nguvu  yako,  najua wanilinda,  huniachi. Shika mikono yangu  niongoze, Mpaka nimalizapo safari        hii!  

169.Rafiki Bora yu Mbinguni

1. Rafiki bora yu mbinguni,  duniani rafiki haba,  sababu hapa mapatano  yanavunjika upesi. Kwa hiyo mimi  nasema: Rafiki bora ni  Yesu.

167.Ni sikukuu Ile

1. Ni sikukuu siku ile ya  kumkiri mwokozi! Moyo umejaa tele,  kunyamaza huwezi. Siku kuu! Siku kuu! ya kuoshwa dhambi  zangu kuu. Hukesha na kuomba tu,  ananiongoza miguu. Sikukuu! Siku kuu! Ya kuoshwa  dhambi  zangu kuu. 2. Tumekwisha kupatana  mimi wake, Yeye wangu,  na sasa nitamwandama,  nikiri neneo la Mungu. Siku kuu!... 3. Moyo tulia kwa Bwana  kiini cha raha yako,  huna njia mbili tena: Yesu ndiye njia yako. Siku kuu! ….. 4. Nadhiri yangu ya mbele  nitaiweka daima,  hata ije siku ile  ya kuonana salama.       Siku kuu!

166.Wamwendea Yesu

1. Wamwendea Yesu  kwa kusafishwa,  na kuoshwa  kwa damu ya Kondoo? Je neema yake  umemwagiwa? Umeoshwa  kwa damu ya Kondoo? Kuoshwa, kwa damu  itutakasayo ya Kondoo; Ziwe safi nguo nyeupe  mno: Umeoshwa  kwa damu ya Kondoo? 2. Wamwandama daima Mkombozi na kuoshwa  kwa damu ya Kondoo? Je, waishi kwake  msulibiwa? Umeoshwa  kwa damu ya Kondoo? Kuoshwa.. 3. Atapokuja Bwana arusi  uwe safi kwa damu ya  kondoo. Yafae kwenda Mbinguni  mavazi  yafuliwe  kwa damu ya kondoo. Kuoshwa…. 4. Yatupwe yaliyo na  takataka,  na uoshwe kwa damu ya  Kondoo Huoni kijito chatiririka  na uoshwe kwa damu ya  Kondoo? Kuoshwa….  

165.Mimi ni Mtoto Mdogo tu.

1. Mimi ni mtoto mdogo tu     na nguvu sinayo.     Nataka kwenda     mbinguni    na njia sijui. 2. Nitapotea kabisa  katika makosa Usiponisaidia Mwokozi ee Yesu. 3. Ulikuwa Mtoto mdogo      kwaajili yangu. Nakupa moyo wangu  huu,  uwe mali yako. 4. Naomba utuangalie,  nishike mkononi! Mimi nitakufuata,  tufike nyumbani.

164.Tumekujia Bwana Wetu

1. Tumekujia Bwana wetu      kujiweka mkononi      mwako,     tuwe wako, hata milele     twakushukuru na     twakusifu.    Mwokozi wetu, utukubali,    utuongoze njia ya mbingu. 2. Twataka kubatizwa leo  kwa Jina lako, tuwe  Wakristo. Umetukomboa na sisi  ulipokufa pale Golgota,  na kwamba wewe upo  karibu, unasikia kuomba kwetu. 3. Twakupambia mioyo leo,  ingia, Mfalme wa utukufu! Utupe sisi nuru yako  tuwe mwanga katika  dunia. Pokea leo mioyo yetu,  tunajitoa kwako wenyewe. 4. Tunakuomba sasa, Bwana,  usitutie majaribuni. Utuongoze siku zote,  tukufuate wenye imani. Mwisho tufike kwenye enzi  kuu, tuipokee taji ya  mbingu.  

163.Mungu Upokee Moyo Wangu

1. Mungu upokee  moyo wangu wote,  niwe mtoto wako,  siku zangu zote. Nikufuate Wewe  nisikuache tena,  nishike siku zote,  ulivyotuagiza. Unisaidie mimi,   hata kufa kwangu. 2. Msalabani pako, Yesu naanguka,  uliyenifia  hata mimi pia. Yaondoe makosa  yatoweke kabisa,  nipate kuwa safi  kwa damu yako bora. Unisaidie mimi Hata kufa kwangu. 3. Roho Mtakatifu,     unanipa nguvu,    niweze kushinda    majaribu yote,   naomba: utawale   kataika moyo wangu,   Shetani, hata kufa,    asinishinde mimi.  Unisaidie mimi,  hata kufa kwangu. 4. Baba, Mwana, na Roho  uliye mmoja tu,  niliye maskini  nakuomba sana:  Unikubali sasa,  katika ubatizo,  futa makosa yangu  kwa maji haya bora. Unisaidie mimi,  hata kufa kwangu.  

162.Bwana Twakuletea

1. Bwana, twakuletea  mtoto huyu,(watu hawa)  tukijua  amri yako ya mwisho  uliyowapa mitume: Watu wote wabatizwe,  watakao kuwa wako. 2. Neno hili ni kubwa     tulilopewa na Yesu:   Atakaye kufika     katika ufalme wako,    hana budi kuzaliwa     tena kwa maji na Roho. 3. Pokea kondoo wako Mchunga mwema Bwana Yesu Umwongoze mbinguni (Waongoze mbinguni)  ndiwe njia na uzima. Umpe kukutegemea  (wape kukutegemea)  apate kukutengamana  (wapate kutengemana). 4. Baba, tunakusihi  ukubali wimbo wetu,  usikie maombi  tunayokuomba sasa. Andika jina la mtoto (Andika majina yao)  katika kitabu chako!  

161.Watumwa Yesu

1. Watumwa waYesu     jitayarisheni,    shikeni neno la Yesu     kesha kila siku. 2. Tengenezeni taa,      wekeni mafuta,     jifungeni muwe mbele,     hata kukimbia. 3. Omba usikome     ninakuja sasa,    angalia nawaonya,    hima njooni kwangu. 4. We utaokoka,    ukikaa kwake,    kutazama uso wake   utavikwa taji 5. Bwana huandaa    wateule wake,    awachukue mbinguni,    karamuni mwake.  

160.Maisha Ya Duniani

1. Maisha ya duniani  ni mafupi,  hata siku ni chache,  zinapita hima na kutoweka  wala hazirudi,  zinatokomea. 2. Vivi hivi kila mmoja      tunakwenda     mbinguni kwake Mungu,     mbele ya kiti chake     cha hukumu      kila mtu atapewa haki     yake. 3. Tunakwenda huko sote  na waamini  waamini waenda bila  woga Kwani wanaye Bwana  wanaingia nchi takatifu. 4. Ee ndugu, twendeni sote  kwake Mungu. Ulimwengu wapita,  utaangamia na dahambi  zako,  usipokubali nawe  waangamia. 5. Basi ndugu tujikabidhi  kwa Mungu tuwapo bado  hai,  kwani tukipuuza tutapotea,  hatutaepuka hukumu  milele.  

159.Mbinguni, Mbinguni

1. Mbinguni, mbinguni Kuna mji mwema.     /:Wapendeza sana,         ni wake Mungu,:/ 2. Milango ya mjini   ni dhahabu tu, /: mungu ndiye jua  anaung`aza.:/ 3. Ugonjwa hauko,  kufa hakuna.    /:Wenyeji wa humo       ni wa kweli tu:./ 4. Waimba usiku  hata na mchana /: Wakimsifu Bwana    Mungu wetu tu.:/ 5. Wote waimbao  wana furaha. /:Wang`azwa na damu  ya Bwana Yesu.:/ 6. Vijana sikieni  wote kwamba.   /:Twapendwa na Yesu,   Bwana wa mbingu.:/ 7. Twendeni kuingia  wote mjini, /:Tupewe uzima  na Bwana wetu!:/  

158.Liko Pumziko la Mioyo

1. Liko pumziko la mioyo,  amka wee unayechoka Unaugua kama mfungwa  kwa shida za moyo wako Umtazame Kondoo wa  Mungu atakuchunga kwa furaha Uache mzigo enenda. Vita nzuri yamalizika,  safari yabaki kidogo  inayokusumbiua mno. 2. Mungu ametuchagulia  pumziko lisilo mwisho Amelitengeneza kale,  mtu hajazaliwa bado,  kufa kwa mfurahisha Mponya,  tupate pa kupumzika. Aita, anaalika  mioyo inayokaa na shida,  msikawie njooni leo! Ingieni pumzikoni! 3. Ninyi mshindwao na  mzigo  mlemewao na uzito Rukeni kimbieni hima,  tokeni pangoni mmwenu,  msienende kwa kuinama Mponya anawaambieni: Mimi ni pumziko lenu,  ninyi wana wote wa  Mungu. Popote mwalizwa na shida,  kwa Yesu mwanyamza           kimya! 4. Hapo pumzikeni rahani,  wasi wasi hatunao. Shikeni neno hili jema: Pumzikeni Yesu yuko! Shikeni mabawa upesi,  karukeni kama ndege Wako jamaa wanangoja, Furahi moyo, sh...

157.MJini ni Mbinguni

1. Mjini ni mbinguni kwa  Mungu, hakuna mabaya na shida,  waongofu wengi wamejaa  wanaomsifu Mwana   Kondoo         Mbinguni,mbinguni         mjini mbinguni        kwa Mungu         ndio mji wa       kutupendeza. 2. Wateule wengi wa huko  wanaongazwa na Yesu,  huko kuna furaha yetu. Jua lake ni la uzima. Mbinguni,… 3. Moyo wangu una furaha  ya kwenda mbinguni kwa  Mungu. Bwana univute uliko,  kiaga chako kitimie!  Mbinguni,…. 4. Kitambo kidogo kipite  na mimi nifike mbinguni Bwana wangu Yesu   nakuomba: Ukoo wangu wote ufike  mbinguni,…   

156.Umejengwa Juu Yerusalemu

1. Umejengwa juu  Yerusalemu,  ninakutamani,  Moyo wangu ukikutamani,   wataka kupita milima na   mabonde,  kuruka kama tai, Uache ulimwengu   uingie kwako. 2. Siku nzuri! Ninaingojea  ifike upesi. Niache dunia niende  mbinguni kwa shangwe. Nimrudishie roho Mwokozi Bwanangu, aipokee vema,  aipe uzima. 3. Mara moja roho itakwenda  kufika mbinguni,  ikiacha uzima wa hapa  kwa nguvu ya Mungu. Yapelekwa na gari  kama Eliya mkuu,  malaika waibeba  vizuri kwa shangwe. 4. Nikifika kule Paradiso,  mwisho huu ni mwema. Roho yangu yajaa furaha,  kinywa husifu tu. Wateule huimba  nyimbo nzuri nyingi,  hawaachi kumsifu Mungu Mwenye enzi.

155.Ondokeni Tunaitwa

1. Ondokeni! tunaitwa  na walinzi wa juu  mnarani Yerusalemu, amka wee! Ni usiku wa manane,  yuaja Bwana wa arusi,  wanawali wako wapi? Amkeni upesi! Kaziwasheni taa. Haleluya! Fuateni arusini  kwenda kumpokea        Bwana! 2. Sayuni anasikia,  moyo waruka kwa furaha,  yu macho anaondoka. Mponya wake anashuka  mbinguni mwenye  utukufu,  aleta mwanga wa kweli,   taji yake yaja  na Mwana wa Mungu. Hosiana! Twafuata kwenye shangwe  tukale karamu yake. 3. Waimbiwa nyimbo nzuri  kwa misemo ya watu wote  na ya malaika mbinguni. Tukifika mjini kwako  kwenye milango ya malulu  tutakuimbia nasi. Furaha kama hii  haijasikiwa duniani. Nasi sasa tunaimba,  tunakusifu, Ee Bwana.  

154.Ninataka Kuingia

1. Ninataka kuingia  mjini kwa Mungu. Nitashinda, nitakaza  mwendo nifike,  nikishikwa na shida,  nikichoka njiani, Yesu unaniambia: “Uningojee!” 2. Naitwa na Yesu Kristo  enzini mwake.  Nakimbia, kukawia  hakuna faida,  wote wachelewao  hawapati taji. Mimi sitaki kingine  ila uzima. 3. Elekeza macho yangu  mlangoni pako. Niongoze, nipe nguvu,  ninapochoka. Ninapojaribiwa,  ninaposingiziwa, Yesu, unisaidie  Nisikuache. 4. Mkono wako unishike  nisianguke. Najiona kuwa mnyonge,  nguvu i kwako, Neno lako, ee Yesu,  linanipa uzima. Nikifika, nitaimba, “Umeniponya!”  

153.Ninapenda Kwenda Zangu

1. Ninapenda kwenda zangu  nimwone Mwokozi  wangu. Moyo wangu watamani  kuambatana na Yesu /: na kumsifu milele.:/ 2. Ninapenda kusikia  nyimbo za malaika wote. Ningekuwa na mabawa  ningeruka leo hivi /: mpaka Sayuni               kwake.:/ 3. Ninapenda kuingia  pale penye utukufu,  penye nyumba za  dhahabu  nimwone Mwokozi  wangu   /: na furaha za         mbingu:/  4. Ninapenda kuona  uzuri wa Paradiso. Nikifika nitapata  tunda lake tamu sana, /: Yesu, nipeleke juu! :/  

152.Mahali pa Raha

1. Mahali pa raha  ya moyo wapi? Akukingiaye  mabaya nani? Dunia haina makimbilio,  nisiposhindwa  na makosa yangu.    /: Sipo sipo hapa sipo        mbinguni ni ngome         ya moyo wangu.:/ 2. Iache dunia,  uone ngome,  unapofurahishwa  moyo wangu. Ni Yerusalemu  unaojengwa  na mawe mazuri  ya dhahabu tu.      /:Ndiko, ndiko,       ndiko ngome       na makimbilio        ya moyo wangu.:/ 3. Mwangani kwa Yesu    ni raha tamu,  hakuna makosa  na shida huko. Vinubi na sauti  za nyimbo nzuri  zinaufurahisha moyo  huko.   /:Raha, raha, raha       tamu     mbinguni kwa Yesu       naitamani.:/  

151.Ee moyo Wangu Hima

1. Ee Moyo wangu, hima,  enenda mbinguni! Ulimwenguni humu  hapana raha. Mchungaji wetu Yesu  achungapo kondoo  ni penye raha kuu. Enenda mbinguni! 2. Yeye akupokee, Mungu Baba yako,  akuketishe pake  katika enzi kuu. Atakuvika nguo  za wongofu wa Mungu,  akupa raha kuu. Enenda mbinguni! 3. Nakutamani sana Mwana Kondoo Mungu! Ningepata mabawa  ningeruka pale,  wanaposhangilia  malaika wake Mungu  katika raha kuu. Enenda mbinguni! 4. Mapenzi yako Bwana  ndizo haja zangu, Utakalo lolote  nami nitatenda. Naingojea siku  utakayoniita,  nipate raha kuu! Enenda mbinguni!  

150.Ahimidiwe Mwamba Wangu

1. Ahimidiwe mwamba wangu,  ahimidiwe ngome yangu,  wema wake wapita vyote  duniani. 2. Aturuzuku kila kitu,  atugawia mema kwetu  wema wake wapita  vyote  duniani. 3. Upendo wake mwingi  sana,  katutolea Mwana wake,  wema wake wapita  vyote  duniani. 4. Katika Yesu, Mwana  wake, Twapatanishwa naye Baba, Wema wake wapita  Vyote  duniani. 5. Ashukuriwe Mungu     wetu,    sifa zote ni zake Bwana    wema wake wapita   vyote     duniani.  

149.Chini ya Bawa Lako

1. Chini ya bawa lako,  ee Yesu nifiche Unipe raha kwako  kwenye mambo yote. Na uwe yote kwangu,  hekima shauri,  na siku zangu zote  niwe na amani. 2. Nisamehe makosa  nioshe kwa damu,  unipe nia safi  na mapenzi mapya. Wakubwa na wadogo  ututunze sote,  na kwa amani yako  tupate furaha.   

148.Mungu Baba Mungu Mwana

1. W:Mungu Baba, Mungu Mwana, Mungu Roho, twakusifu   twakushangilia sote, umejifunua kwetu  kwa upendo,  kwamba wanadamu  wakujue wote. K:/:Mungu wetu W:Anapenda tuwe     Wake K: Dhambi zetu W:Tuache, tumfuate.:/ 2. W: Mungu Baba wewe   uliumba vyote, Mbingu, dunia  navilivyomo vyote,  watu ndege na  wanyama uliumba, Jua  mwezi na nyota  vyakutukuza. K:/: Mungu wetu:/ 3. W: Mungu Mwana,  wewe ulikuja kwetu,  ukaishi kama  mwanadamu kweli,  ukateswa na kubeba  dhambi zetu,  kwamba sisi tupate  wokovu kweli. K:/: Mungu Wetu:/ 4. W: Mungu Roho,  uliye kiungo chetu,  wakusanya  na kuita watu wote,  tufundishe kumjua Bwana wetu,  na utukufu wake  hata milele. K:/: Mungu wetu:/  

147.Mtakatifu wewe Mungu

1. Mtakatifu Wewe,         Mungu Mwenye enzi,          jua likitoka tutakutukuza         wee.         Mtakatifu Wewe          wa huruma nyingi,        Mwenyezi Mungu wa         Utatu. 2. Mtakatifu Wewe,    waliokoka     wakusujudia Wewe     huko daima.   Makerubi wote    wakuinamia,   Mwenyenzi Mungu wa       Utatu. 3. Mtakatifu Wewe,   siri wajificha,  macho yetu hayawezi kukutazama, Wewe peke yako Mtakatifu kweli, Mwenyenzi Mungu wa    Utatu. 4. Mtakatifu Wewe   Mungu Mweny enzi,  kazi zako zakusifu kila  mahali. Mtakatifu Wewe  wa huruma nyingi, Mwenyenzi Mungu wa     Utatu.Amen.  

146.Mwenyezi, Mwenyezi, Mwenyezi

1. Mwenyezi, Mwenyezi, Mwenyezi, Jina lako litukuzwe sana. Amini, Amin. Hata ulimwengu wetu  uteketezwe kwa moto. Nazo nyumba zetu,  ziimbe utakatifu wake, Haleluya, Haleluya.  

145.Bwana Wema Wako Popote

1. Bwana wema wako popote  hata mbinguni huko juu. Bwana wema wako popote  hata mbinguni huko juu.      /: Na welekevu, na              welekevu/:  wako huenea na  mawinguni  na welekevu wako  huenea na mawinguni.         :/ /:Haleluya x4         Haleluya x 2/: