92.Ukiwa na Vichache

1. Ukiwa na vichache
Umtolee Bwana, 
kwani akiba yako 
ataiongeza. 
Vipaji vyako haba.
Yeye hakatai,
kidogo kwako wewe,
kwake kitazidi!


2. Vile vile na moyo 
umtolee Bwana!
Ndivyo vipaji vyema 
vinavyompendeza.
Kwani sisi wenyewe, 
alitukomboa, 
akiuawa Yeye 
kwa kuwambwa mtini.


3. Ukiwa na ubaya 
umwambie Bwana!
Ukishandana nao, 
atakutakasa.
Damu aliyotoa, 
ndiyo itoshayo, 
kuosha wakosaji, 
hata wewe hivyo.


4. Vitu vya mali nyingi 
umtolee Bwana! 
Alitoka mbinguni 
kusumbuka hapa. 
Alikufa mwenyewe 
kwa ajili yako, 
nawe hutoi chako 
kwa ajili yake?


5. Wakristo na tutoe 
    shukrani kwa Mungu. 
    Hiyo ndiyo shukrani 
     ya wokovu wetu.
    Injili yake Kristo, 
     ienee pote!   
     Kwa ushuhuda wetu  
     watu waokoke.



 

Comments

Popular posts from this blog

17. Tuimbe na kusifu

32 Kitoto Mpenzi Lala Wee

143.Mungu ni wa Utukufu