114.Amefufuka Katika Wafu
1. K: Amefufuka katika wafu,
akiwa na utukufu.
Kristo pekee,
ndiye mwenye nguvu.
W:/:Yeye limbuko
la waliolala,
tena ni mwisho
wa nguvu ya mauti
kwetu.:/
2. K: Hii ni habari iliyo kweli,
iletayo udhahiri
Yapasa wote,
tuache mashaka.
W:/: Yesu usifiwe,
Wewe pekee ndiwe
ustahiliye kushika
mamlaka yote:/
3. K:Kristo u Bwana
mwenye uweza
Shetani ummeshinda,
kazi yote umeimaliza.
W:/:Uhimidiwe
Ewe Bwana pekee,
Utupokee tunapokuja
kwako Bwana.:/
4. K: Tuutangaze ushindi,
wake,
mataifa waje kwake,
wafahamu utukufu
wake,
W:/:Asante, Bwana,
Kwa ushindi wako
kwa watu wako.
Shetani hana nguvu
tena:/
Comments
Post a Comment