103.Moyo Yafurahie Yafanywayo
1. Moyo yafurahie,
yafanywayo leo:
Mwanga umetokea
gizani mwa kufa.
Mwokozi kalazwa,
tutakapozikwa,
roho ikiisha
kurudi mbinguni.
2. Alipozikwa Yeye
adui acheka.
Lakini akashindwa:
Kristo afufuka.
Atokea shujaa
bendera mkononi,
kwani ameteka
mateka ya mwovu.
3. Ni jambo kubwa
hili lenye furaha kuu.
Sitaogopa sasa
uchungu wa kufa,
na yote mengine
yatakayoteka
mali nipewayo
na Yesu Mwokozi.
4. Namshika siku zote
Mwokozi wangu mkuu.
Yeye ni kichwa chetu
sisi tu viungo.
Dunia makosa
Shetani na kufa
Yeye kawashinda,
nami namfuata.
5. Afika furahani
nami nitafika,
Sitaona huzuni
Na shida zozote.
Mkubwa wangu Yesu
ataniakingia
vinavyonidhuru,
Yeye ngao yangu.
6. Nitakapoingia
mbinguni, naona
andiko la furaha
Linasomwa hivi:
Ashindaye kule
Aingia hapa,
anayejidhili
atakuzwa hapa!
Comments
Post a Comment