84.Nimshangilie Bwana Wangu
1. Nimshangilie
Bwana wangu
na kumwimbia
Mkombozi,
katukomboa msalabani,
nisifu pendo lake kuu.
Haya mwimbieni Yesu,
amekubali mateso
katukomboa
msalabani,
tusifu pendo lake kuu!
2. Tumsifu Yeye
Mponya wetu
katika ulimwengu huu,
katupatanisha na Baba
tulio wakosaji tu.
Haya mwimbieni...
3. Katuletea mwanga wake,
tulikaa katika giza,
wokovu ukaonekana,
kamshinda mwovu,
ni shujaa!
Haya mwimbieni….
4. Na tumtukuze Bwana
wetu,
tumtumikie kwa bidii,
na atawale apendavyo,
na sisi sote tuta mtii!
Haya mwimbieni……
Comments
Post a Comment