Posts

170.Yesu Wangu Simwachi

1. Yesu wangu simwachi,     kwani amenikomboa. Akitoa maisha,  kulipa madeni yangu. Sasa namwelekea,      Yesu wangu          simwachi! 2. Yesu wangu simwachi,  siku zote za duniani. Nimempa yangu yote,  ayashike mikononi.       Sasa namwelekea…. 3.Yesu wangu simwachi,      anichunga kwa upole    malishoni vizuri, mwenye shangwe  ampendaye: Sasa namwelekea…..  

168.Shika Mikono Yangu

1. Shika mikono Yangu,  niongoze,  mpaka nimalizapo  safari hii. Nikiwa peke yangu  napotea. Po pote uendapo  nipeleke! 2. Tuliza moyo wangu,  uwe kimya,  nikiona furaha au  majonzi,  unitulize sana,  ndimi wako,  sitaki neno tena, ila hilo. 3. Nisipoona leo nguvu  yako,  najua wanilinda,  huniachi. Shika mikono yangu  niongoze, Mpaka nimalizapo safari        hii!  

169.Rafiki Bora yu Mbinguni

1. Rafiki bora yu mbinguni,  duniani rafiki haba,  sababu hapa mapatano  yanavunjika upesi. Kwa hiyo mimi  nasema: Rafiki bora ni  Yesu.

167.Ni sikukuu Ile

1. Ni sikukuu siku ile ya  kumkiri mwokozi! Moyo umejaa tele,  kunyamaza huwezi. Siku kuu! Siku kuu! ya kuoshwa dhambi  zangu kuu. Hukesha na kuomba tu,  ananiongoza miguu. Sikukuu! Siku kuu! Ya kuoshwa  dhambi  zangu kuu. 2. Tumekwisha kupatana  mimi wake, Yeye wangu,  na sasa nitamwandama,  nikiri neneo la Mungu. Siku kuu!... 3. Moyo tulia kwa Bwana  kiini cha raha yako,  huna njia mbili tena: Yesu ndiye njia yako. Siku kuu! ….. 4. Nadhiri yangu ya mbele  nitaiweka daima,  hata ije siku ile  ya kuonana salama.       Siku kuu!

166.Wamwendea Yesu

1. Wamwendea Yesu  kwa kusafishwa,  na kuoshwa  kwa damu ya Kondoo? Je neema yake  umemwagiwa? Umeoshwa  kwa damu ya Kondoo? Kuoshwa, kwa damu  itutakasayo ya Kondoo; Ziwe safi nguo nyeupe  mno: Umeoshwa  kwa damu ya Kondoo? 2. Wamwandama daima Mkombozi na kuoshwa  kwa damu ya Kondoo? Je, waishi kwake  msulibiwa? Umeoshwa  kwa damu ya Kondoo? Kuoshwa.. 3. Atapokuja Bwana arusi  uwe safi kwa damu ya  kondoo. Yafae kwenda Mbinguni  mavazi  yafuliwe  kwa damu ya kondoo. Kuoshwa…. 4. Yatupwe yaliyo na  takataka,  na uoshwe kwa damu ya  Kondoo Huoni kijito chatiririka  na uoshwe kwa damu ya  Kondoo? Kuoshwa….  

165.Mimi ni Mtoto Mdogo tu.

1. Mimi ni mtoto mdogo tu     na nguvu sinayo.     Nataka kwenda     mbinguni    na njia sijui. 2. Nitapotea kabisa  katika makosa Usiponisaidia Mwokozi ee Yesu. 3. Ulikuwa Mtoto mdogo      kwaajili yangu. Nakupa moyo wangu  huu,  uwe mali yako. 4. Naomba utuangalie,  nishike mkononi! Mimi nitakufuata,  tufike nyumbani.

164.Tumekujia Bwana Wetu

1. Tumekujia Bwana wetu      kujiweka mkononi      mwako,     tuwe wako, hata milele     twakushukuru na     twakusifu.    Mwokozi wetu, utukubali,    utuongoze njia ya mbingu. 2. Twataka kubatizwa leo  kwa Jina lako, tuwe  Wakristo. Umetukomboa na sisi  ulipokufa pale Golgota,  na kwamba wewe upo  karibu, unasikia kuomba kwetu. 3. Twakupambia mioyo leo,  ingia, Mfalme wa utukufu! Utupe sisi nuru yako  tuwe mwanga katika  dunia. Pokea leo mioyo yetu,  tunajitoa kwako wenyewe. 4. Tunakuomba sasa, Bwana,  usitutie majaribuni. Utuongoze siku zote,  tukufuate wenye imani. Mwisho tufike kwenye enzi  kuu, tuipokee taji ya  mbingu.