80.Liko Neno Moja Nipendalo
1. Liko Neno moja nipendalo,
ni chakula cha moyo,
Neno hili linanituliza
nikipatwa na shida:
Kumtazama Bwana Wetu
pale,
atoapo jasho kama damu,
akubalipo mzigo,
Baba aliomtwika
2. Siku zote
namkumbuka yeye,
alivyosulubishwa,
akivumilia taabu kimya
kama mwana wa kondoo.
Nami akanikumbuka
mimi,
akisema: Yamemalizika!
Huko aliniteka,
nami niwe mtu wake.
3. Bwana wangu,
u mwenye huruma,
mimi ni mkosaji tu;
nilipokuwapo penye giza
wewe ukatokea,
ukamtafuta kondoo wako,
kabla mimi sijakusikia.
Watoa ukombozi
unipao uhuru.
4. Ndimi huru lako,
Bwana Yesu,
wewe ndiwe Bwanaangu.
Jina lako, bora liung’aze
moyo wangu vizuri.
Amani yako nikae nayo,
Siku zangu zote mpaka
kufa.
Ndivyo ninavyoomba,
Bwana unikubali.
Comments
Post a Comment