101.Moyo Wangu Amka Hima

1. Moyo wangu amka hima,
   Jua limetokea.
   Ondoka usingizini, 
   mpokee mponya wako, 
   atokaye kaburini, 
   kashinda nguvu za kifo 
   watu wafurahishwe.


2. Fufuka pamoja naye, 
uyaache mabaya!
Maliza mwenendo wako 
ukimngojea Yesu, 
aliyekwenda mbinguni.
Kwa hiyo nawe ufanye 
yampendezayo yeye.


3. Ukiwa na wasiwasi
Yesu anauweza:
Ukipatwa na huzuni,
Yeye furaha yako.
Umtwike Bwana mzigo.
Usisumbuke: yu hapa, 
kwani amefufuka.


4. Usimwogope shetani, 
kifo hata kuzimu
Shida za kufa nyepesi
Mwokozi Yesu ni mzima.
Shuja wetu haondoki, 
awagombea wanyonge 
wanaomtumaini.



 

Comments

Popular posts from this blog

17. Tuimbe na kusifu

32 Kitoto Mpenzi Lala Wee

143.Mungu ni wa Utukufu