71.Wajibu Mwema watoka Kwako
1. K: Wajibu mwema
watoka kwako
Bwana mwenye
utukufu.
Neno jema ndilo Jina
lako.
W: /: Yesu ni mwanzo
wa kazi shambani,
tena ni Bwana,
wa nguvu kwa utume
wetu.:/
2. K: Watendakazi mwako
shambani,
uwape matumaini.
Nazo nguvu wakiwa
kazini.
W: /: Watende yote kwa
uaminifu,
wawe makini,
huduma isiharibike.:/
3. K: Wapate heri
kuyasikia uliyoyaagizia.
waje nao kutuhubiria.
W:/: Tena kazini
wakaelezee Neno
kwa wazi, na kweli
ya uzima wako.:/
4. K:Wajihadhari
wawe na hamu,
kushika na kufahamu.
Jina lako likawarehemu.
W:/: Ni wachungaji,
Wajue hilo tu
Si watawala.
Bwana , ujifunue kwao.:/
5. K: Unawtuma katika kundi,
Kwa bidii na juhudi.
Nasi kwao tuwe mashahidi.
W:/: ushangiliwe
kwa neema yako,
na kundi lako
lijue lina viongozi.:/
Comments
Post a Comment