62.Uamke Kwetu Tena Roho

1. Uamke kwetu tena Roho
wa mashaidi wale wa 
kwanza,
waliokesha siku zote,
waliomshinda yule adui,
wakihubiri Neno la Yesu
kwa watu wa ulimwengu
wote.


2. Uwashe moto wa upendo,
Uendelee pote kuwaka.
Peleka watu mavunoni,
Wanaofanya kazi kwa bidii.
Bwana mwenye mavuno,
Tazama:
Watenda kazi yako ni haba.


3. Mwanao ametuagiza
kuomba hivi kwa jina lake,
na sisi wanafunzi wake,
twashika neno lake kwa bidii.
Twaomba hivi kwa moyo
 wote.
Ee Bwana usikie, ufanye!


4. Utume watu wengi sana,
walitangaze Neno kwa nguvu.
Tusaidie, tuokoe;
Ufalme wa shetani uishe.
Usimamishe, Bwana wa
Mbingu,
Ufalme wako
Ulimwenguni!


5. Utume mwema na uende
mahali popote huku
nchini.
Wa dini zote waingie
kundini mwako mwa 
wateule.
Amsha nao Wana wa ahadi
Na wa Imani zote wakutii.




Comments

Popular posts from this blog

17. Tuimbe na kusifu

32 Kitoto Mpenzi Lala Wee

143.Mungu ni wa Utukufu