127.Karibu Kwangu Roho
1. Karibu kwangu Roho
ingia moyoni,
uliyeniletea
uzima na raha.
Roho Mtakatifu
wa Baba na wa Mwana
ufananaye nao
ukaaye nao.
2. Unafundisha watu
kuomba vizuri,
wapate kusikiwa
na Mungu mbinguni.
Unatuombea,
hukomi, mpaka Mungu
atende mambo yale
uliyoyaomba.
3. Wafurahisha moyo,
hupendi huzuni,
tukiwa matesoni,
unatutuliza.
Wazungumza nasi
kwa Neno lako tamu,
unatia mioyo
furaha ya kweli.
4. Unatufanya sisi
kuwa usharika,
hutaki tugombane
na kuchukiana.
Wanaopigana
unawapatanisha,
wataka wapendane
Wakristo wowote.
5. Ulinde nchi yetu,
serikali yetu,
tukae na amani
duniani humu.
Uwape wakubwa,
pamoja na wadogo
uchaji na akili,
wampendeze Mungu.
6. Katika mwendo wetu
utupe na sisi
nguvu, tumshinde mwovu
akitujaribu.
Utusaidie,
tushike njia yako
na mwisho tufe vema
tufike kwa Mungu.
Comments
Post a Comment