107.Kumekucha ni Mzima
1. Kumekucha, ni mzima
Yesu aliyefufuka.
Kaburi lake wazi,
Kufa hakumshiki Yesu.
Sina woga na kifo,
Yesu amefufuka.
2. Kumekucha, ni mzima
Yesu, aliyefufuka!
Tunaitwa nduguze,
sababu anatupenda.
Tusiachane naye,
Yeye aliyeshinda.
3. Kumekucha, ni mzima
Yesu aliyefufuka.
Kamaba zitufungazo
Zimekwisha funguliwa
Mwili wangu uoze,
sina woga na kufa!
Comments
Post a Comment