108.Tumfurahie Daima
1. Tumfurahie daima,
Yesu aliyefufuka
Haleluya! Haleluya!
Giza haliwezi kukaa,
Jua limelifukuza.
Haleluya! Haleluya!
Haleluya! Haleluya!
Haleluya!
2. Naona Moyo wa Maria,
Unashangalia sana,
Haleluya! Haleluya!
Nayo mioyo yetu sisi,
Inapiga shangwe nyingi!
Haleluya!.....
3. Jeraha zake za kufa,
Zatupatia uzima,
Haleluya! Haleluya!
Na sasa anatawala
Katika enzi ya Baba.
Haleluya!...
4. Mwokozi hakuogopa,
Kuvuka maji ya kufa.
Haleluya! Haleluya!
Atupa nasi moyo mkuu.
Tuongoze tufikee juu!
Haleluya!....
Comments
Post a Comment