Posts

Showing posts from July, 2023

43 Yesu Ulale

1. K: Yesu, ulale, W: Haleluya K: Yesu, ulale W: Haleluya K: Tulia, Mwana, W: Haleluya K: Tulia, Mwana, W: Haleluya K: Mwana wa Maria, W: Haleluya K: Mwana wa Daudi, W: Haleluya K: Shina la Yesu W: Haleluya, K: Haleluya, W: Haleluya       Mtoto, Ee,       Mwema tu,       Kila anayekuamini,       Utamgawia amani tu. 2. K: Lala, Ee Yesu,    W: Haleluya    K: Lala, Eee Yesu,    W: Haleluya    K: Ufumbue macho,    W: Haleluya    K: Ufumbue macho,    W:Haleluya    K: Mzao wa Ibrahimu,    W: Haleluya,    K: Mwana wa Isaka,   W: Haleluya    K: Mrithi wa Yakobo,    W: Haleluya    K: Haleluya    W: Haleluya      Mtoto Ee…..  

42 llitoka Nuru Kuu

Never shone a light so fair Mtunga maneno: J. F. Crosby 1823-1915 Asili:N.S56. Sauti:S.S&S. 2 Mtunga sauti: R. Lowry 1. llitoka nuru kuu, kuliko nuru zote. Na huo wimbo wa juu wapita nyimbo zote; Ndiyo habari tukufu, ya Kristo wa utukufu, awajia wapole; Ni Mungu pamoja na sisi, Imanueli. 2, Mwaka huandama mwaka, wimbo huu na uimbwe; Wapenda kukumbusha, mzee na wanawe, ndiyo habari tukufu, ya Kristo wa utukufu, awajia wapole; Ni Mungu pamoja na sisi, Imanueli 3. Twafurahi siku hii ijavyo kila mwaka; Nasi tufanye bidii huku tukikumbuka, Ndiyo habari tukufu, ya Kristo wa utukufu, awajia wapole; Ni Mungu pamoja na sisi, Imanueli.

41 Tumepata Mwokozi

Asili ya wimbo Kibena. Sauti T.M. 17 1. K: Tumepata Mwokozi sasa W: Bwana Yesu K: Ee, ee! W: Tumepata Mwokozi sasa. 2. K: Duniani hatuna mtu W: Hata mmoja K: Ee? ee! W: Duniani hatuna mtu. 3. K: Tutafute msaada wapi W: Huku chini K: Ee, ee! W: Tutafute msaada wapi? 4. K: Peke yetu tungepotea. W: Peke yetu. K: Ee, ee! W: Peke yetu tungepokea 5. K: Yuko Yesu peke yake tu, W: Yuko Yesu. K: Ee, ee! W: Yuko Yesu peke yake tu. 6. K: Asema, Nakufia wewe W: Mwanadamu, Mtunga wimbo: Y. Chambile na F. De Zwart K: Ee, ee! W: Asema, Nakufia wewe. 7. k: Katumwagia damu yake W: Msalabani. K: Ee, ee! W: Katumwagia damu yake. 8. K: Katulipia dhambi sisi W: Wakosaji. K. Ee ee! w: Katulipia dhambi sisi. 9. K: Katupatanisha na Mungu, W: Haleluya. K’ Ee ee! W: Katupatanisha na Mungu. 10. K: Kwa sababu hiyo ni wake, W: Mali yake. K: Ee, ee! W: Kwa sababu hiyo ni wake. U.K: Haniachi mtoto wake, W: Haniachi. K: Ee, ee! W: Haniachi mtoto wake.

40 Tushangilie Sote

Sauti ya Kibarbaig, T.M. 13 Mtunga maneno: Mudimi Ntandu 1922 K: Tushangilie sote W: Kila mtu. K: Mwana wa Mungu akaja W: Hata kwetu. K: Tumjue Mungu Baba W: Wa huruma. K: Usiku wa manane W: Shangwe kubwa K: Alipozaliwa Kristo W: Awe Mfalme. K: Pale katika mji W: Wa Daudi. K: Kwenye kondoo hata ng'ombe W: Bethlehemu. K: Na akaitwa kwa Jina W: K: Nalo Vesu Mwokozi W: K: Mungu nasi. Hakika ni Mwokozî W: K: Mwenye enzi Tu patı we uzîma W: Wa milele. K: Na kumtumikia daima W: Siku zote. K: Maana kwake sasa tumemwona W: Mungu wetu. K: Na hîvyo hata Roho W: K: Mtakatifu Njonî kwa hiyo tumsifu W: Bila mwisho.

39 Umezaliwa Mtoto

Sauti ya kishambala .T.M 12 Mtunga maneno na sautl: H. Mavula 1. K: Tumezaliwa mtoto, tumezaliwa mtoto. Ni Bwana Vesuz Mwana wa Mungu Atakayewachunga kondoo.    W: Amezaliwa mtoto. Asante, Bwana Mungu. /: Ulivyoona kondoo wako, huku chini ya mbingu, hawana Mchungaji.:/ 2. K: Wewe Mama Mariamu, wewe Mama Mariamu, Utaziona huzuni nyingi atakapotimiza sheria.   W: Wewe Mama Mariamu, na umshukuru Mungu, /: Alivyoona kondoo wake, huku chini ya mbingu, hawana Mchungaji. :/ 3. K: Ni furaha yetu kubwa, ni furaha yetu kubwa, Tukitumiwa Mwokozi Yesu ili atupiganie vita.   W: Ni furaha yetu kubwa, na tumshukuru Mungu. /: Alivyoona kondoo wake, huku chini ya mbingu, hawana Mchungaji.:/

38. Sauti imetoka Mbinguni

1.  K: /; Sauti imetoka mbinguni; W: Sauti imetoka mbinguni. :/ K/:Ahubiri malaika wake Mungu; W; Ahubiri malaika wake Mungu:/ 2 K: /: Ninyi watu acha kuogopa; W; Ninyi watu acha kuogopa:/ K: /; Nawaletea h a bari, furahini; W; Nawaletea habari, furahini:/ 3 K: /: Leo amezaliwa Mwokozi; W; Leo amezaliwa Mwokozi:/ K;/; Kazaliwa Kristo ni Mwokozi wenu:/ W: Kazaliwa Kristo ni Mwokozi wenu;/ 4. K; /: Mtamwona kalazwa, horini; W: Mtamwona kalazwa, horini. :/ K; /: Mtamwona huyo amevikwa nguo; W: Mtamwona huyo amevikwa nguo:/ 5. K:/: Nanyi makundi, huko mbinguni; W: Nanyi makundi, huko mbinguni. :/ K: Saidia kushukuru Mungu w/etu; w: Saidia kushukuru Mungu wetu.:/ 6’ K: Utukufu wa Mungu mbinguni; Utukufu wa Mungu Mtunga maneno: B. Mung'ong’o mbinguni. K: /: Kawapa watu amani duniani; W; Kawapa watu amani duniani. :/ 7. K: /: Hakika Mungu ametuona; W: Hakika Mungu ametuona. ;/ K: /: Tufurahi, tumfurahie Mwokozi; W: Tufurahi, tumfurahie Mwokozi. :/ 8. K: /: Na wenzetu waone, Ee Mungu; W: N...

37 Sote Tufurahi

Asili: Kihaya, T.M 6 Mtunga maneno: W. Kyakajumba 1. K: Sote tufurahi, W: habari ni njema K: Njooni nyote wahi, W: tupate uzima Sasa yametimia yaliyotabiriwa Mwokozi kazaliwa. 2. K: Kule Bethlehemu W: Yesu kazaliwa K: Mama Mariamu W: alivyoambiwa. Sasa ... 3. K: Kumbe, huyo Mwana W: kalazwa horini K: Huyo Yesu Mwana W: akawa shidani. Sasa ... 4. K: Mwana atiiye W: ni Bwana shujaa, K: Kwake tuwe wana, W: ni Mponya dunia. Sasa ... 5. K: Jeshi la mbinguni W: katoa Injili. K: Watu malishoni, W: kaona ni kweli. Sasa .. 6. K: Mungu yupo nasi W: katika dunia. K: pendo kwa waasi, W: katoa kwa nia. Sasa ... 7. K: Raha na tushike, W: tunaye Masihi K: Haya twende kwake W: sauti zasihi. Sasa ... 8. K: Wote wenye Mwana W: wanao uzima. K: Yeye ndiye Bwana, W: atoa karama. Sasa ... 9. K: Nyota yatunuka W: shinani mwa Yese. K: Bwana atukuka, W: akatutakase. Sasa ... 10. K: Sasa, ndugu, nyote W: tangaza neema. K: Waje kwake wote W: tupate rehema. Sasa ...

36 Mwema ni Bwana Mbinguni

Sauti: Enre, Enre, Ehre sei Gott in der “hoeche. Wimbo: Luka 2:14 N.K. 34, P.B. 11330 Mtunga sauti: F. Silcher, 1825 Mwema, mwema, mwema ni Bwana mbinguni, na utengemano kwa watu wanaompendeza, kwa watu wanaompendeza. Mwema ni Bwana mbinguni. Mwema ni Bwana mbinguni, nchi itengemane, watu wapendezwe, wote wakampendeze Bwana. Mwema, mwema, mwema ni Bwana mbinguni na utengemano kwa watu wanaompendeza kwa watu wanaompendeza!

35 Tazama Nawatangazia

Sauti: Siehe, siehe, ich verkuendige euch. Wimbo: Luka 2:10-11, N.K. 33 Mtunga sauti: G. p. Weimar, + 1800 Tazama, nawatangazia, nawatangazia, nawatangazia, shangwe kubwa, shangwe kubwa, shangwe kubwa, shangwe kubwa. Shangwe, shangwe kubwa inayokuja, kwa watu wote, wa koo zote; inayokuja, inayokuja. Amezaliwa leo, Bwana Mwokozi, ndiye Kristo Yesu, Bwana wa mjini! mwa Daudi, Bwana wa mjini mwa Daudi, wa mjini mwa Daudi!

34. Wakristo Furahini

Sauti na wimbo: freut euch, ihr lieben Christen. L.B.W. 87. N.K. 32 Mtunga Sauti: L. Shroeter, 1587 Asili: 1540 1. Wakristo furahini, furahini sana! Mwaipigiwa leo mbiu yenu njema! Malaika wanaimba huko juu mbinguni, /: wanaimba vizuri sauti ya kushangaa! ะ/ 2. Hivi wanavyoimba: Furahini nyote! Acheni kuogopa, tazameni nyote kwani amezaliwa Mwokozi wa pekee: /: ni Bwana Yesu Kristo, Mwana Mungu wetu:/ 3. Shangilieni nyote na kusikiliza. Wapigieni nyote mbiu na sauti kuu. Mungu katupa sote mtoto wa mbinguni, /: kwa kutupenda sisi amekuja kwetu. ะ/

33. Niende na Wachungaji

Sauti na wimbi: Mit den Hirten will ich gehen. Gr. M.H. I 39, N.K. 31 Mtunga sauti: A. Rische, 1891-1906 Mtunga maneno: E. Quandt, 1835-1911 1. Niende na wachungaji nimtazame Mponya wangu, kazaliwa duniani kwa kunipenda mimi. 2. Nimwimbie na malaika, niusifu utukufu. Anautengemaza, kila moyo umpende. 3. Nikawaze na Maria jambo hili la ajabu: Aacha mwili mzuri, achukua wa kimtu. 4. Nimpelekee vipaji na watambuzi wa nyota, na nîmpe mali yangu, hata uzima nimpe. 5. Nakupenda, u Mwokozi, nikumbuke siku hii. Uje mwangu moyoni, uufanye kikao.

32 Kitoto Mpenzi Lala Wee

Sauti: Kijerumani. T.B. 17, P. B. Ill 7.2, N.K. 30 Asili: Kadriga 1706 Mtunga maneno: Schubert, 1734-1791 Wimbo: Schlaf wohl, du Himmelsknabe du 1. Kitoto mpenzi lala wee, Kitoto wa mbingu! Malaika wakupepea ulale kwa raha. Nasi maskini wachunga tunakubembeleza wee. Lala, ulale: Kitoto wee, ulale. 2. Maria kwa upendo mkuu amlaza vizuri. Yosefu amekaa kimya ili asimwamshe. Na wanyama wa nyumbani wamenyamaza kabisa: Lala, ulale: Kitoto wee, uiale. 3. Yesu utakapokua, watakuumiza. Kilimani pa Golgota, utasulibishwa. Kwa hiyo sasa lala tu! Kwa raha na utulivu! Lala, ulale: Kitoto wee, ulale.

31 Malaika Njooni Toka Juu

Sauti na wimbo: Vom Himmet hoch, o Engel kommt. Wimbo: Froehliche Weihnacht ueberall Asili: Koeln, 1623. T.B. 4, N.K. 29 1. Malaika njooni toka juu! Oye, oye, tazama, tazama kitoto. Imbeni, pigeni panda. Haleluya! Haleluya! Nyimbo za Yesu na Maria! 2. Kwa sauti kuu mwimbieni! Oye, oye, tazama, tazama kitoto. Kwa vinanda na vinubi. Haleluya! Haleluya! Nyimbo za Yesu na Maria! 3. Tungeni nyimbo tamu mno, Oye, oye, tazama, tazama kitoto, kupita ndege wa anğa. Haleluya! Haleluya! Nyimbo za Yesu na Maria! 4. Utamu wa nyimbo zenu, Oye, Oye, tazama, tazama kitoto. Umbembeleze, alale. Haleluya! Haleluya! Nyimbo za Yesu na Maria! 5. Watu na watengemane, Oye, oye, tazama, tazama kitoto. Na Mungu tumpe shukrani! Haleluya! Haleluya! Nyimbo za Yesu na Maria!

30 Mpige Mbio Wachungaji

Sauti na wimbo: O laufet, ihr Hirtern Asili: Silesia, T.B. 5, N.K. 28 1. Mpige mbio, wachungaji mpige mbio wote, Chukueni na filimbi na zumari pia. Mpige mbio wote, mpige mbio wote Bethlehemu kwenye hori walishwamo ng'ombe. 2. Mumtazame mtoto mzuri aliyezaliwa, na wazazi wake mtoto wako huko naye. Ni Yosefu baba na Maria mama, mwanamwali mzuri sana kama malaika juu. 3. Hebu njooni, ee jamani mİ ete nguo nzuri! Tumlazeni mtoto wetu kwa uzuri wote! Twakubembeleza wewe mtoto lala! Lala Yesu mpenzi wetu twakubembeleza.

29. Siku ya Furaha Popote

Sauti: Kiingereza. N.K. 27. P.B. III 26 1. Siku ya furaha popote, Sauti za kusifu zavuma! Duniani, nyumbani nyimbo za furaha kuu: Siku ya furaha popote, Sauti za kusifu zavuma! Wote na tushiriki furaha yetu, mwanga wa ulimwengu waja toka juu. Siku ya furaha popote, Sauti za kusifu zavuma! Duniani, nyumbani nyimbo za furaha kuu: Siku ya furaha popote, sauti za kusifu zavuma! 2. Siku ya furaha popote, Sauti za kusifu zavuma! Duniani, nyumbani, nyimbo za furaha kuu: Siku ya furaha popote, Sauti za kusifu zavuma! Azaliwa Mesiya kwetu duniani: Tulio wa gizani, tuwe wa Mwanga. Siku ya furaha popote... 3. Siku ya furaha popote, Sauti za kusifu zavuma! Duniani, nyumbani nyimbo zafuraha kuu:           Siku ya furaha popote,         Sauti za kusifu zavuma! Wote na tushiriki furaha yetu, mwanga wa ulimwengu waja toka juu. Siku ya furaha popote, Sauti za kusifu zavuma! Duniani, nyumbani nyimbo za furaha kuu: Siku ya furaha popote, sauti za kusifu zavuma!...

28.Amkeni Upesi

Sauti: Kijerumani. Wimbo: fhr Hirten erwact. T.B. 10, N.K. 26 Asili: Paderborn 1- Amkeni upesi wachunga kondoo! Malaika washuka, habari watupa: Furaha karibu, Mwokozi aja! 2. Wachungaji njooni, tumtafuteni! Akiwa zizini pigeni filimbi. Furaha karibu... 3. Wachungaji hima washika njia. Pamoja wamwona mamaye, babaye. Furaha karibu ... 4. Wamjua upesi mtoto wa mbingu. Wapiga magoti kumwimbia nyimbo. Furaha karibu ...