123.Siku Hii Tuliyomwona
1. Siku hii tuliyomwona
akipaa juu mbinguni,
alifia wakosaji,
kurudia enzi yake.
2. Huko shangwe yake
nyingi
milangoni pa milele.
Kashinda makosa, kufa,
Yeye Mfalme mwenye
nguvu.
3. Ajapokwenda mbinguni,
alipenda ulimwengu.
Akikaa kitini mwake,
sisi atutunza hapa.
4. Tazama mkononi mwake
alama za pendo lake!
Awatia mibaraka
watu na makundi yake.
5. Na sisi atuombea
akikaa utukufuni,
na atutengenezea
makao tukae naye.
Comments
Post a Comment