104.Yesu Amefufuka

1. Yesu Amefufuka, 
sitakuogopa kufa.
Amefufuka, naye 
atanifufua mimi.
Atanipa mwili mpya: 
ni tumaini langu.


2. Yesu amefufuka, 
anapatawala pote.
   Nami nitatawala 
  pamoja naye milele.
  Atimiza agano:
  ni tumaini langu.


3. Yesu amefufuka, 
yanipasa kumngojea.
Mwenye kumtegemea
Bwana wetu, ataona 
rehema yake Mungu:
Ni tumaini langu.


4. Yesu amefufuka, 
naweza kumtumikia, 
na shindana na tama, 
moyo wangu uwe safi
Atanisaidia:
Ni tumaini langu.


5. Yesu amefufuka, 
siwezi kutengwa tena 
na Yesu Bwana wangu.
Kwa mateso au furaha.
Vyote havinishindi:
Ni tumaini langu!


6. Yesu amefufuka, 
ni mlango wa kuingia 
furahani mbinguni.
Nitatulizwa nikifa, 
nikiweza kusema:
U tumaini langu!



 

Comments

Popular posts from this blog

17. Tuimbe na kusifu

32 Kitoto Mpenzi Lala Wee

143.Mungu ni wa Utukufu