Sauti: Kijerumani. T.B. 17, P. B. Ill 7.2, N.K. 30
Asili: Kadriga 1706
Mtunga maneno: Schubert, 1734-1791 Wimbo: Schlaf wohl, du Himmelsknabe du 1. Kitoto mpenzi lala wee,
Kitoto wa mbingu!
Malaika wakupepea
ulale kwa raha.
Nasi maskini wachunga
tunakubembeleza wee.
Lala, ulale: Kitoto wee, ulale.
2. Maria kwa upendo mkuu
amlaza vizuri.
Yosefu amekaa kimya
ili asimwamshe. Na wanyama wa nyumbani
wamenyamaza kabisa:
Lala, ulale: Kitoto wee, uiale.
3. Yesu utakapokua,
watakuumiza.
Kilimani pa Golgota,
utasulibishwa.
Kwa hiyo sasa lala tu!
Kwa raha na utulivu!
Lala, ulale: Kitoto wee, ulale.
Comments
Post a Comment