125.Tazameni Anapaa
1. Tazameni, napaa,
mwenye kushinda vita,
gari lake ni mawingu,
ndipo anapopita,
malaika wa mbinguni
wakimwimbia Bwana,
Amekaribishwa sasa,
kwa kufurahi sana.
2. Ni nani anayepaa,
wote wakimsifu?
Ndiye Bwana mwenye
enzi,
ndiye Mungu wa Safu,
aliyeteseka kwanza
mle katika mti,
kwa kifo chake
mwenyewe,
akashinda mauti.
3. Akaaga watu wake,
na akawabariki
akapaa mawinguni
na wakimwangalia,
chini hutenda ya Mungu,
yote yakitimia,
kazi yake imekwisha,
kwake amerejea.
4. Ni kuhani wetu sasa,
yumo na damu yake,
katika patakatifu
twapatanishwa kwake,
Amefanya ukombozi
kuondoa dhambi zetu,
Mungu amekubali
ndiye sadaka yetu.
5. Mwili ameuinua
huo wa ki-Adamu,
ndani yake sisi sote
pia tuna sehemu
Mungu na Mtu pamoja
yuko huko enzini
twaamini Bwana,
kwamba
tutakwenda mbimguni.
Comments
Post a Comment