78.Mwokozi Wangu Umekosa Nini?
1. Mwokozi wangu
umekosa nini?
Wahukumiwa kama mwuaji.
Umeshtakiwa makosa
Mangapi uliyotenda?
2. wapigwa sana
miiba taji lako,
umetemewa
mate,
watukanwa,
wanyweshwa nyongo
tena siki kali.
3. Sababu gani
unateswa hivi?
Makosa yangu yanakuumiza;
mateso haya yako yanipasa,
mimi mkosaji.
4. Ajabu kubwa
sana tendo lako;
mchungaji unateswa kwa
ajili ya kondoo,
Bwana
unawalipia watumwa wako.
5. Tuliopokuwa mateka
wa mwovu,
nawe ukaja ukatukomboa.
Tulistahili kufa kwa
Milele,
Ukatufia.
6. Mwokozi wangu
nifanyaje mimi,
niitangaze pote sifa yako?
Nakufuata nikutumikie
maisha yote.
Comments
Post a Comment