110.Haleluya, Haleluya

1. Haleluya, Haleluya,
Sauti na mioyo juu, 
tumwimbie Mungu 
nyimbo, 
tumsifu na furaha,
Aliyemwaga damuye 
kwa ulimwengu wote, 
amefufuka kifoni
Sasa Yesu Mwokozi. 


2. Minyororo yake kifo 
imekatikatika pia, 
na katika wafu wote
Yee mzaliwa wa kwanza
Yesu ameshinda sasa, 
 nasi twashinda naye.
Ametupatia nasi 
uzima wa milele.


3. Kristo afufuka kwanza 
   nao wengi baadaye.
  Atakapokuja tena, 
   watatokea naye, 
   mavuno yatakuwako 
   mwisho wa ulimwengu, 
   watafika furahani 
    wote watakatifu.


4. Mwokozi amefufuka, 
nasi tutafufuka.
Tunyeshee kama mvua 
neema yako ee Bwana.
Tutafute yaliyo juu, 
siyo ya ulimwengu, 
na uzima tutapewa 
naye Kristo kwa Mungu.


5. Tumsifuni, tumsifuni
Mungu wetu, apaswa.
Tumsifuni na Mwokozi, 
aliyeshinda vita.
Tumsifuni naye Roho, 
kisima cha mapenzi. 
Tumsifuni Mungu wetu, 
ni Utatu wa enzi.



 

Comments

Popular posts from this blog

17. Tuimbe na kusifu

32 Kitoto Mpenzi Lala Wee

143.Mungu ni wa Utukufu