Posts

Showing posts from June, 2023

27. Amezaliwa Mtoto

Sauti: Kîjerumani. Wimbo: zu Bethlehemu geboren Gr. M.H. I 29.N.K. 25 Asili: Koeln 1. Amezaliwa mtoto mjini Bethlehemu. Nimemchagua yeye, niwe mali yake! Oye, oye, niwe mali yake! 2. Nataka kuingia pendoni mwake yee na kumtolea moyo hata vyangu vyote, Oye, oye, hata vyangu vyote. 3. Kwa moyo wote safi nataka kumpenda shidani, furahani hata kila wasaa. Oye, oye, hata kila wasaa. 4. Unikubali hivyo, naomba kabisa nikuishie Wewe, leo na daima! Oye, oye, leo na daima!

26 Nchi Mbingu Furahi

Sauti na wimbo: Freu dich, Erde' und Sternenzelt Mtunga sauti: A. Zahn, 1877 Asili: Bohemia, N.K. 24. L.B.W. 57 1. Nchi, mbingu furahi! Haleluya! Amekuja Mwokozi, Haleluya! Mwana wake Mungu amekuja kwetu, Mwana amekuja kwetu. 2. Toka shina la Yese, Haleluya! Tawi limechipuka, Haleluya! Mwana wake Mungu... 3. Neno lake Mwenyezi, Haleluya! Limekuja duniani, Haleluya! Mwana wake Mungu...

25 Mungu ni wa Utukufu

Sauti: Imechukuliwa kwa Cantate "Gott İst Licht". Wimbo: Hark! The herald angels sing.T.B. 15, N.K. 23, L.B.W. 60 Mtunga sauti: F. Mendelssohn, 1840 Mtunga maneno: Ch. Wesley, 1739 1. Mungu ni wa utukufu panapo mbinguni juu, na kwao wampendezao duniani raha kuu. Sikieni nchi zote huko mjini Bethlehemu: /: Kristo amezaliwa, Bwana wetu daima. :/ 2. Watu na malaika wote wanamtukuza Yesu, ashukaye toka mbingu kuwa kama maskini. Akaacha enzi yake, akavaa unyenyekevu: /: Kristo amezaliwa,..:/ 3. Asifiwe Mungu Mwana na Mwokozi wa watu, mleta mwanga na uzima Yesu mshinda kuzimu, Mfalme wa utengemano huko mjini Bethlehemu. /:Kristo amezaliwa,...:/

24. Ulimwenguni Pote

Sauti: Veni redemptor gentium Wimbo: Gott sei Dank durch alle Welt P.B. I 125, R.L. 46, L.B.W. 28, N.K. 22 Mtunga maneno: H. Held, 1620-1659 Mtunga sauti: S. Ambrosius, Mailand 397 1. Ulimwenguni pote asifiwe Mungu mkuu amemtuma Mwokozi, wakosaji wapone. 2. Zamani wazee wale wameona hamu kuu, waondoshwe makosa na kumpata Mwokozi. 3. Abrahamu, Yakobo na watu wa Sayuni walimngojea sana, sasa ametujia. 4. Karibu Mponya wangu niondolee woga. Ujitengenezee njia moyoni mwangu. 5. Safisha nyumba yako umfukuze Shetani, yule nyoka wa kale. Nikutumikie wee!

23. Msifuni Mungu Wakristo

Sauti Korn mt her, ihr liebston Schwesterlein. Wimbo: lobt, Gott, ihr Christen. 1. Msifuni Mungu, Wakristo, aliyetukuka, atufungulia mbingu /:kumtoa mwanawe:/ 2. Atokaye kifuani pa Mungu Babaye, alala sasa kitoto /: kitupu, maskini. ะ/ 3. Anyonya kwa mama yake, maziwa chakula, kwa kweli anatulisha /Chakula cha mbingu.:/ 4. Ageuza hali yake, avaa mwili wetu na sisi anatuvika /: uzima wa Mungu. ะ/ 5. Akawa mtumwa, na mimi naitwa kibwana, niwe nduguye na mtoto /: wake Mungu Baba ะ/

22. Yesu Kitoto Kizuri

Sauti nd wimbo: Du lieber heif'ger, N.K. 20 frommerChnst P.B III 18,Gr.M.H. 132 Mtunga sauti: G. Siegert, 1822 Mtunga maneno: E.M. Arndi. 1808 1. Yesu kitoto kizuri, umetujia watoto utupe mioyo mizuri, tuwe watoto wa Mungu. 2. Ee Mwanga toka mbinguni, umetufikia sisi, tupate mwanga wa kweli, tuunganishwe na Mungu. 3. Mpenzi wangu Mtakatifu, umezaliwa duniani: furaha iko kwa wote, kwa wakubwa na wadogo. 4. Unibariki ni mdogo, moyo unisafishie, ondoa taka ya roho, upendo wetu uzidi!

21. Watoto Njooni Bethlehemu

Sauti na wimbo: Ihr Kinderlein kommet, P.B.I uk 16 b, N.K.19. Mtunga sauti: J.A.P. Schultz, 1794 Mtunga maneno: Chr. V. Schmidt, 1. Watoto njooni, Bethlehemu, njooni zizini kuona makuu Mungu aliyotutendea leo, watoto waone furaha kubwa. 2. Twaona kitoto kîzuri hapa, wazee wamtazama, wanafurahi. Wachungaji wote wamwangukia, malaika wa mbingu wanamwimbia. 3 Pigeni กาagoti na wachungaji? Wakubwa, wadogo tumnyenyekee! Tuimbe na sisi kwa furaha kuu, nyimbo za kumsifu Mwokozi Yesu’ 4. Watoka mbinguni utuokoe, waona uchungu sababu yetu, leo wazaliwa mwana kikiwa. Halafu wateswa, unatufia. 5. Twapenda kukupa mioyo yetu, twataka kukutumikia vema. Takasa mioyo ikupendeze, tupate kufika k\wako mbinguni-

20. Njooni wachungaji Bethlehemu

  Njooni wachungaji Bethlehemu. Njooni kumtazama Mtoto mzuri. Mwana wa Mungu amezaliwa. Baba amtuma awakomboe Msiogope! 2. Twende Bethlehemu tukaone tulivyoambiwa na malaika. Tuyaonayo tutatangaza na kutukuza kwa nyimbo Haleluya! 3. Kweli malaika wametanganza  Furaha kubwa kwa wachungaji. Sasa po pote patengenezwe na watu wote watapendezwa Furahini!

19. Usiku Mtakatifu

Mtunga maneno: Fr. J. Mohr, 1792-1848 Mtunga sauti: F. Gruber, 24.12. 1818 1, Usiku mtakatifu! Wengine walala wakeshao ni Yosefu tu na Maria waliomlinda Yesu mwana mzuri Yesu mwana mzuri 2. Usiku mtakatifu! Wachunga wapewa habari nzuri na malaika, zienezwe popote sasa: Yesu M pony a kaja Yesu Mponya kaja. 3. Usiku mtakatifu! Siku ya furaha imetuangaza Kimungu tumeupewa ukombozi Kristo amefika Kristo amefika.

18. Umati wa Yesu

Jauti; Adeste Fideles. Gr. M.H. I 43, R.L. 52 L0.W. 42, N.K. 16 Mtunga maneno: John F. Wade, 171 1786 1. Umati wa Yesu, njooni kwa furaha msikie habari ya sikukuu! Mwana wa Mungu azaliwa kwetu. Njooni tumtukuze! Njooni tumtukuze! Njooni tumtukuze! Yesu Kristo! 2, Mbinguni malaika wamwimbia wote na wote wakaao kwake Mungu- Mungu ni mkuu, aliyetupenda. Njooni tumtukuzel ... 3. Tumsifu Mwokozi Yesu siku zote, aliyezaliwa kwetu leo. Anatujia atufurahishe. Njooni tumtukuze!...

17. Tuimbe na kusifu

Tuimbe na kusifu Kwa nyimbo za furaha: Yesu Bwana wetu  amezaliwa leo Zizini Bethlehemu. Furaha ya mioyo. Mponya na mwokozi, Tunakusifu 2. Nakutamani sana, uliyetoka juu. Ee Mwokozi mwema tuliza moyo wangu, unipe neema yako, Kitoto cha huruma. Univute juu, univute juu. 3. Rehema zake Mungu ni nyingi, alimtuma Mw/ana wake Yesu, awakomboe watu, atufanyie njia, tufike tena kwetu. Kwetu ni kwa Mungu, kwetu kwa Mungu. 4. Na watu wakaao katika giza wote wanakungojea Wewe Mwokozi wetu, na kukufurahia uliyetukomboa. Yesu Bwana wetu twakutukuza.

16. Tunakuamkia Yesu

Sauti na wimbo; Gelobet seist du, Jesu Christ. L.B.W. 48, N.K. 14, Dkt. Martin luther、483 1546 Mtunga maneno. 1. Tunakuamkia Yesu, tunakupa pongezi. Umezaliwa kikiwa, malaika wakuabudu, Uwe nasi! 2. Mwana wa Mungu wa pekee, Yeye ni mgeni wetu, Anajiunga na sisi Mfalme W3 kale na kale! Uwe nasi! 3. Ashikaye ulimwengu ashikwa na Maria! Ni mtoto mdogo na mchanga! Tena ni Bwana wa mbingu! Uwe nasi! 4 Nuru ya milele aja kuleta mwanga wake. Aondoa giza lote; tuwe watoto wa mwanga. Uwe nasi! 5 Kwetu akawa maskini kwa kutuhurumia, tupate mali ya mbingu, tuwe watoto wa Mungu. Uwe nasi! 6. Amefanya haya yote kwa kuwa atupenda. Kwa hiyo furahini tu na tumshukuru daima! Uwe nasi!

15. Tawi Limechipuka

 Sautî na wimbo: Es ist ein Ros'entsprun^en. P.B. I 228, LB. W. 58, N.K. 13 Asili: Koeln. 1599 1. Tawi limechipuka shinani mwa Yese, kama tulivyopashwa habari na wazee. Likatoa ua wakati wa usiku, lilipochanua. 2. Isaya alitaja ua hilo zuri. Ni Yesu, Mponya wetu, Maria alimzaa. Usiku mtulivu. Uwezo wake Mungu umefanya hivi. 3. Na ua hili dogo lanukia vyema; lang'aa kama jua giza lafukuzwa. Ni Mwana wa Mungu pia mwana Adamu; Mwokozi wa watu. 4. Siku ya kufa kwetu Yesu tuongoze, tuiache dunia, twende furahani mbinguni kwa Mungu Pale tutakusifu Pasipo kukoma.

14. Siku ya Furaha (Aliyozaliwa Yesu)

Sauti: O sanctissima, P.B. I 233, N.K. 12 Wimbo: O du froehliche, o du selige. 1. Siku ya furaha, siku ya uzima aliyozaliwa Yesu. /: Tulipotea Yesu akaja. Furahini, furahini, Wakristo!:/ 2. Siku ya furaha, siku ya uzima aliyozaliwa Yesu. /:Yesu ashuka, atuokoe. Asili: Sicily, 1803 Mtunga maneno: J. D. Falk, 1786-1826 Furahini, furahini, Wakristo! :/ 3. Siku ya furaha, siku ya uzima aliyozaliwa Yesu. /:Malaika wote wamsifu Mungu. Furahini, furahini, Wakristo!:/

13 Salamu Yesu Bwanangu

Sauti: Es ist gewisslich P. B. 1 115, L. B. W. 321, N. K. 11 Mtunga maneno: Paul Gerhardt, 1768-1826 Asili: Karne 1400 1. Salamu Yesu Bwanangu,  Wewe uzima wangu.  Nimekujia naleta vyote ulivyonipa: Tangu mimi sijaumbwa,  umenitengenezea,  ukombozi wa moyo. Ni moyo na mwili wangu,  hata na mawazo yangu,  ndiyo heshima yangu.  3. Uvuli mzito wa mauti,  ulinifunikiza:  Umenitokea jua,  waniangaza moyo. 2. Umezaliwa Bwanangu kwa ajili ya mimi; umenipenda kabisa,  umenipa wokovu. Wewe Bwana umenipa nuru,  raha na uzima.  Nakushukuru Bwana.

12. Njooni Tumheshimu Yesu

Saut1. Den die Hirten lobeten sehre Wimbo: Kommt und lasst uns Christum ehren. N. K. 10, P. B. I 230 Mtunga sauti: Johann Eccard, 1S91 Mtunga maneno: Paul Gerhardt, 1607-1676 1. Njooni, tumheshimu Yesu, tumtolee sifa zetu. Tumwimbie kwa furaha, sisi watu wa Yesu. 2. Baba amemtuma Mwana atuletee uzima, utakaopewa watu wenye shida na kufa. 3 Moyo wake watupenda kwa upendo amekuja, aokoe wenye dhambi wasishindwe na mwovu. 4. Nuru imetutokea, Yesu akiponda kichwa cha adui wetu mkali anayetudanganya. 5. Tutabarikiwa kweli, tukishika Neno hili, tukimsifu Bwana Yesu kwa vinywa na mioyo. 6. Mwana mzuri Bwana Yesu, twakuomba tupeleke pale wakuimbiapo malaika nyimbo nzuri.

11. Natoka Leo Mbinguni

Sauti na wimbo: Vom Himmel hoch da komm ich hier, P. B. 1160, Mel. 185, A. H. 27. L. B.W. 51, N. K. 9 Asili: V. Schumann, Leipzig, 1539 Mtunga maneno: Martin Luther, 1483-1546 I. Natoka leo mbinguni' naleta habari njema habari yenye furaha kwa ninyi na watu wote. 2. Amezaliwa kitoto, na mwanamwali Maria, ni mtoto mzuri na mwema, awaletea furaha. 3. Ni Yesu, Mwana wa Mungu, Mwokozi wa ulimwengu, Atakayekuondoa makosa yote na shida. 4. Awapa wote wokovu, uliowekwa na Mungu, nnkae nanyi mbinguni pamoja nasi milele. 5. Alama yenu iwe hii: Zizini mtoto maskini aliyevikwa viguo, naye ni Bwana wa mbingu. 6. Tumsifuni sisi sote, tuwafuate wachunga, tuyaone yale makuu, tuliyopewa na Mungu. 7. Yesu unipendezaye, ugeuze moyo wangu, uwe nyumba yako nzuri, nisikuache daima. 8. Tumsifu Bwana wa mbingu, aliyemtoa Mwanawe. Tumwimbie kwa furaha, pamoja nao malaika.

10. Bwana Anakuja

1. Bwana anakuja twendeni kumlaki, Bwana Mungu wa majeshi. Iwasheni mioyo tukampokee, huyo Mwenye utukufu. /:Karibu Bwana, njoo:/ Shinda pamoja nasi. 2. Wewe ndiwe Mfalme, Mfalme wa mbinguni, utulishe wenye njaa. Wewe ndiwe กาพลกga sisi tu vipofu, tufanye tuone tena. /:Karibu Bwana... 3. Wewe ndiwe njia, tutakufuata' turudi kwa Baba /etj. Wewe ndiwe kwe!i, utuangazie, tusije tukapotea. /:Karibu Bwana... 4. Hosana, Hosana, huyo mbarikiwa, anakuja kwetu sisi. Aja kutulisha na kutugawia matunda ya ukombozi. /:Karibu Bwana...

9. Faraja Tumaini Langu

0 du mein Trust und suesses Hoffen Sauti: T.B. 2, Gr. M. H., I, 5 Mtunga wimbo: Wilhelm Osterwald 1820-1887 Mtunga sauti: Johann Wolfgang 1. Faraja, tumaini langu usiniache gizani. Moyo ni wazi kukungoja, Ee Yesu uniingie. Furaha ya mbingu na nchi, Mwana Adamu na Mungu; Ee nuru kutoka mbinguni, an- gaza moyo wangu huu. 2. Mtoto mpendwa, nakuomba, chagua moyo wangu huu, ufanye kuwa hori lako ukalazwe humo wewe. Ih nipate mwisho mwema wa shida yangu na vita. Zaliwa ndani yangu Yesu, na ndani yangu ukue. 3. Mwokozi wangu utulize, tumaini hili kubwa. Ukija nitakupokea kwa roho nyenyekevu, hii. Uweza wangu wote pia wakungojea kwa uchu. Nataka kukutumikia: Njoo, Yesu usikawie.

8. Amekuja Mwokozi

Sauti na wimbo: Kibena, T.M.3 1. K: /: Amekuja W: Mwokozi.:/ K: /: Ufalme wa juu karibu. W: Amekuja Mwokozi.:/ 2. K: /: Geukeni W: mioyo.:/ K: /: Watatupwa wenye kiburi. W: Geukeni mioyo. :/ 3. K /: Shoka lipo W: Shinani,:/ K: /:Mti usiozaa wakatwa. W: Shoka lipo shinani.:/ 4. K: /: Ana ungo W: mkononi, :/ K: kupepeta ngano yake. W: Ana ungo mkononi.:/ 5. K: /:Yatachomwa W: Makapi,:/ K: Ngano yawekwa chanjani. W: yatachomwa makapi :/ 6. K: /:Nabatiza W: kwa maji, :/ K: Yeye, hubatiza kwa Roho. W: Nabatiza kwa maji. :/ 7. K: /:Mbele yake şifa i, :/ W: Şifa i,:/ K: Kumfungulia viatu, W: Mbele yake sifai. :/ 8. K: /: Elekea W: Mbinguni,:/ K: Kristo katufanyia Njia. W: Ya kwendea mbinguni.:/

7. Moyo Wangu Sikiliza

Sauti na wimbo: Froehlich soil mein Herze spingen. L. B. W. 46, P. B. 1163, N.K. Mtunga sauti:LJ. Crueger, 1656,1598- 1662. Mtunga maneno: Paul Gerhardt, 1607-1676 1. Moyo wangu sikiliza, habari njema hii, ya wokovu mkubwa. Sikia kuimba kwao malaika na watu: "Yesu azaliwa." 2. Mponya amekuja leo kutoka mbinguni, aokoe watu. Mungu wetu ameshuka, akawa mwana mtu kwa ajili yetu. 3. Na sasa yumo zizini, aita: "njooni, hima kwangu wote, Nawaondolea ninyi uchungu wowote, muwe na furaha" 4. Basi tumwendee hima wakubwa wadogo, njooni wote sasa! Yule anayetupenda, tumpende na sisi, awe mwanga wetu. 5. Wenye shida na ukiwa njooni, awape neema yake Mungu, Yeye ana mali nyingi, dhahabu na fedha za mioyo yenu. 6. Ninakaa ufimwenguni lakini napenda kuhamia kwako. Mwisho niwe furahani pamoja na Wewe, ทาwenye utukufu.

6. Wakristo lwekeni Mioyo Tayari

Sauti: N.K. 164. Wimbo: Mit Ernst, o Menschinkinder. P. B. 1 5 & 94 Mtunga maneno: V. Thilo, 1607-1662 1. Wakristo, iwekeni mioyo tayari. Yesu awaingie, ni Mwokozi wenu. Mungu amemtuma kwa neema na rehema, atuletee sisi uzima na nuru. 2. Mwokozi anakuja, mlimieni njia! Mioyo iwe safi acheni matendo yanayomchukiza. Lijazwe kila bönde, milima ipunguzwe mioyoni mwenu. 3. Ukiwa mnyenyekevu, wapendwa na Mungu. Ukiwa na kiburi, utaangamizwa. Ukimtumikia, Mungu kwa mwendo mwema umpendezao yeye, Yesu akupenda. 4. Uniweke tayari niliye maskini, Ee Yesu siku hizi kwa rehema yako. Ingia moyoni, ukinijia sasa. Nami nitakusifu kwa kinywa na moyo.

5 Nikulakije Vema

Sauti: Valet will ich dir geben Wimbo: Wie soil ich dich empfangen pB 159, Mel 8, N. K. 5, S. B. H. 11 Mtunga sauti: M. Mtunga maneno: 1607-1676 Teschner, 1613 Paul Gerhardt. 1. Nikulakije vema Bwana wangu Yesu? Wote wanakungoja wapewe uzima. Nuru yako ing'aze hata moyo wangu. Nijue mambo mema, yakupendezayo. 2. Wamekutandikia maua na nguo. Nami nakuimbia nyimbo za furaha. Moyo ukupendeze kwa sifa na nyimbo ukakutumikie siku zangu zote. 3. Umetoka mbinguni ukawa maskini. Ukaacha furaha utupe uzima. Na tuliponyang'anywa ufalme na raha, Mponya wetu kuturudishia. 4. Nalifungwa na mw0vu: Ukanifungua Nikawa nimetwezwa, ukanitukuza. ’ Ukanifanya mkubwa, ukanipa mali, zisizomalizika, kwa kutu na wezi 5. Umenijia mimi, sababu ya nini? Sababu ya kupenda, uwaponye wote; waonao huzuni, kwa makosa yao, wakijuta kwa kweli, utawapokea 6. Ushike neno hili: Umati wa Yesu, ukiwa na huzuni, na shida popote. Usiogope kitu, wokovu tayari. Anayetufarij...

4. Fungua Milango Yote

Sauti na wimbo: Macht hoch die Tuer P. B. 1226, N.K. 4, L.B.W. 32 Asi": J. A. Freylinghausen, 1704 Mtunga maneno: G. Weissel, is9o 1. Fungua milango yote, yuaja Bwana wa mbingu. Mfalme wa wafalme wote, Mwokozi wa ulimwengu. Atuletea uzima; kwa hiyo tumwimbieni: Tumsifuni Mungu, aliyetuumba. 2. Ni mwenye haki na shujaa, upole mwingi amevaa; Rehema ni taji ya ke, huruma ni fimbo yake: Atuondolea shida. Kwa hiyo tumwimbieni: Tumsifuni Mungu, Mwokozi wetu mkuu. 3. Miji na nchi huchipushwa afikako Mfalme huyu; nayo mioyo huchekeshwa anayoingia Yesu. Ndiye jua la furaha linalotufurahisha. Tumsifuni Mungu mtunza mioyo yetu. 4. Fungua milango yote! Tengenezeni mioyo! Makuti yawe upole, furaha, pendo, amani. Mwokozi atawajia, aleta raha, uzima. Tumsifuni Mungu, ni mwenye rehema. 5.Njoo, Mwokozi wangu Yesu,  nakufungulia moyo.  Uingie na rehema,  nione upole wako.  Uniongoze kwa roho,  nifike kwako mbinguni,  jina lako Bwana  li...

3.Sayuni Ufurahi

Sauti: Seht, er kommt mit Presis gekroent Wimbo: Tochter Zion, freue duch N.K. 3, RB. II 391 Mtunga sauti: G. F. Haendel, 1747 Mtunga maneno: H. Ranke, 1798-1876 1. Sayuni ufurahi. Shangilia Yerusalemu! Yuaja Mfalme wako, mwenye amani kwako. Sayuni ufurahi! Shangilia Yerusalemu. 2, Hosiana Mesiya Utubariki sasa, Jenga ufalme wako Ulimwenguni mwote. Hosiana Mesiya Utubariki sasa. 3. Hosiana pongezi! Twakuamkia Bwana! Kiti cha enzi yako chasimama milele. Hosiana pongezi! Twakuamkia Bwana.

2. Hosiana, Mesiya

Sauti Grosser Gott, wir loben dichz N K. 2 Wimbo: Hosiana 1. Hosiana Mesiya, aingia mjini kwake. Fagieni popote, zipambeni njia zote; Tandikeni maua, aingie na shangwe. 2. Hosiana Mwokozi! Njoo, twakungojea Bwana Tumepamba mioyo, twakukaribisha kwetu. Tunakufungulia, milango ya mioyo 3. Hosiana, ee Shujaa! Utusaidie sisi. Tuwe wako kwa kweli, tukutumikie vema. Kwani hutakubali watu wasiokutii. 4. Hosiana Mfalme mkuu! Uingie kwetu hima! Uliyebarikiwa, Uingie mlango wetu. Hosiana, karibu! Bwana, njoo! Haleluya!

1. Hosiana! Asifiwe

Hosiana! Asifiwe ajaye kwa Jina la Bwana! Hosiana mbinguni! Anakuja kwa Jina la Bwana, Sauti na wimbo: Hosianna, gelobt sei Anakuja kwa Jina la Bwana, Hosiana! Hosiana! Hosiana mbinguni! Hosiana mbingun"