87.Ee, Watoto Njooni
1. Ee, watoto njooni,
njooni Golgota,
mtazameni Yesu
aumizwavyo!
2. Mtazameni huko
Mkamtazame,
Sogeeni kwake,
ametupenda.
3. Sogeeni kwake,
mkamtazame,
mioyo iyeyuke,
mwangukieni!
4. Mioyo imililie
Anayeteswa,
mzigo wetu mkubwa
aukubali.
5. Mzigo wa makosa
ya ulimwengu.
Mpeni nanyi nyote
mioyo yenu!
6. Apata mshahara,
Ni kufa kwake,
Wewe una raha,
Kwake ni kufa
7. Atoa enzi
ya utukufu.
Tuimbe Haleluya
na kumshukuru.
Comments
Post a Comment