112.Leo Siku ya Furaha

1. Leo siku ya furaha,
    Kila mtu ashangilie,
    Kristo Yesu afufuka, 
    ateka adui wote!
    Haleluya!


2. Nyoka wa kale na kifo,
Kuzimu hata ubaya
Vimeshindwa 
na mshindaji
Yesu Kristo Mfalme 
wetu!
Haleluya!


3. Mateka yote ya kifo 
yamekamatwa na Yesu, 
na ufu umenyang’anywa 
naye aliyefufuka!
Haleluya!


4. Adui hawatushiki 
tunakwenda uzimani, 
tunapokunywa naye 
kinywaji kipya milele!
Haleluya!


5. Jua na mwezi na nchi,
Viumbe vyote vya Mungu
Vinafurahiwa leo:
Mfalme wa uongo 
ashindwa!
Haleluya!


6. Kwa hivi tushangilie, 
tumwimbie Yesu Kristo,
Yeye ametuokoa, 
afufuka kaburini!
Haleluya!



 

Comments

Popular posts from this blog

17. Tuimbe na kusifu

32 Kitoto Mpenzi Lala Wee

143.Mungu ni wa Utukufu