150.Ahimidiwe Mwamba Wangu
1. Ahimidiwe mwamba wangu,
ahimidiwe ngome yangu,
wema wake wapita vyote
duniani.
2. Aturuzuku kila kitu,
atugawia mema kwetu
wema wake wapita
vyote
duniani.
3. Upendo wake mwingi
sana,
katutolea Mwana wake,
wema wake wapita
vyote
duniani.
4. Katika Yesu, Mwana
wake,
Twapatanishwa naye
Baba,
Wema wake wapita
Vyote
duniani.
5. Ashukuriwe Mungu
wetu,
sifa zote ni zake Bwana
wema wake wapita
vyote
duniani.
Comments
Post a Comment