168.Shika Mikono Yangu
1. Shika mikono Yangu,
niongoze,
mpaka nimalizapo
safari hii.
Nikiwa peke yangu
napotea.
Po pote uendapo
nipeleke!
2. Tuliza moyo wangu,
uwe kimya,
nikiona furaha au
majonzi,
unitulize sana,
ndimi wako,
sitaki neno tena, ila hilo.
3. Nisipoona leo nguvu
yako,
najua wanilinda,
huniachi.
Shika mikono yangu
niongoze,
Mpaka nimalizapo safari
hii!
Comments
Post a Comment