160.Maisha Ya Duniani
1. Maisha ya duniani
ni mafupi,
hata siku ni chache,
zinapita hima na kutoweka
wala hazirudi,
zinatokomea.
2. Vivi hivi kila mmoja
tunakwenda
mbinguni kwake Mungu,
mbele ya kiti chake
cha hukumu
kila mtu atapewa haki
yake.
3. Tunakwenda huko sote
na waamini
waamini waenda bila
woga
Kwani wanaye Bwana
wanaingia nchi takatifu.
4. Ee ndugu, twendeni sote
kwake Mungu.
Ulimwengu wapita,
utaangamia na dahambi
zako,
usipokubali nawe
waangamia.
5. Basi ndugu tujikabidhi
kwa Mungu tuwapo bado
hai,
kwani tukipuuza tutapotea,
hatutaepuka hukumu
milele.
Comments
Post a Comment