156.Umejengwa Juu Yerusalemu


1. Umejengwa juu 
Yerusalemu,
 ninakutamani,
 Moyo wangu ukikutamani, 
 wataka kupita milima na 
 mabonde,
 kuruka kama tai,
Uache ulimwengu 
 uingie kwako.


2. Siku nzuri! Ninaingojea 
ifike upesi.
Niache dunia niende 
mbinguni kwa shangwe.
Nimrudishie roho
Mwokozi Bwanangu,
aipokee vema, 
aipe uzima.


3. Mara moja roho itakwenda 
kufika mbinguni, 
ikiacha uzima wa hapa 
kwa nguvu ya Mungu.
Yapelekwa na gari
 kama Eliya mkuu, 
malaika waibeba 
vizuri kwa shangwe.


4. Nikifika kule Paradiso, 
mwisho huu ni mwema.
Roho yangu yajaa furaha, 
kinywa husifu tu.
Wateule huimba 
nyimbo nzuri nyingi, 
hawaachi kumsifu
Mungu Mwenye enzi.




Comments

Popular posts from this blog

17. Tuimbe na kusifu

32 Kitoto Mpenzi Lala Wee

143.Mungu ni wa Utukufu