155.Ondokeni Tunaitwa

1. Ondokeni! tunaitwa
 na walinzi wa juu
 mnarani
Yerusalemu, amka wee!
Ni usiku wa manane, 
yuaja Bwana wa arusi, 
wanawali wako wapi?
Amkeni upesi!
Kaziwasheni taa.
Haleluya!
Fuateni arusini 
kwenda kumpokea 
      Bwana!


2. Sayuni anasikia, 
moyo waruka kwa furaha, 
yu macho anaondoka.
Mponya wake anashuka 
mbinguni mwenye 
utukufu, 
aleta mwanga wa kweli,
  taji yake yaja 
na Mwana wa Mungu.
Hosiana!
Twafuata kwenye shangwe 
tukale karamu yake.


3. Waimbiwa nyimbo nzuri 
kwa misemo ya watu wote
 na ya malaika mbinguni.
Tukifika mjini kwako 
kwenye milango ya malulu
 tutakuimbia nasi.
Furaha kama hii 
haijasikiwa duniani.
Nasi sasa tunaimba, 
tunakusifu, Ee Bwana.



 

Comments

Popular posts from this blog

17. Tuimbe na kusifu

32 Kitoto Mpenzi Lala Wee

143.Mungu ni wa Utukufu