161.Watumwa Yesu
1. Watumwa waYesu
jitayarisheni,
shikeni neno la Yesu
kesha kila siku.
2. Tengenezeni taa,
wekeni mafuta,
jifungeni muwe mbele,
hata kukimbia.
3. Omba usikome
ninakuja sasa,
angalia nawaonya,
hima njooni kwangu.
4. We utaokoka,
ukikaa kwake,
kutazama uso wake
utavikwa taji
5. Bwana huandaa
wateule wake,
awachukue mbinguni,
karamuni mwake.
Comments
Post a Comment