164.Tumekujia Bwana Wetu

1. Tumekujia Bwana wetu 
    kujiweka mkononi 
    mwako, 
   tuwe wako, hata milele 
   twakushukuru na 
   twakusifu.
   Mwokozi wetu, utukubali, 
  utuongoze njia ya mbingu.


2. Twataka kubatizwa leo 
kwa Jina lako, tuwe 
Wakristo.
Umetukomboa na sisi 
ulipokufa pale Golgota, 
na kwamba wewe upo 
karibu,
unasikia kuomba kwetu.


3. Twakupambia mioyo leo, 
ingia, Mfalme wa utukufu!
Utupe sisi nuru yako 
tuwe mwanga katika 
dunia.
Pokea leo mioyo yetu, 
tunajitoa kwako wenyewe.


4. Tunakuomba sasa, Bwana, 
usitutie majaribuni.
Utuongoze siku zote, 
tukufuate wenye imani.
Mwisho tufike kwenye enzi 
kuu, tuipokee taji ya 
mbingu.



 

Comments

Popular posts from this blog

17. Tuimbe na kusifu

32 Kitoto Mpenzi Lala Wee

143.Mungu ni wa Utukufu