152.Mahali pa Raha
1. Mahali pa raha
ya moyo wapi?
Akukingiaye
mabaya nani?
Dunia haina makimbilio,
nisiposhindwa
na makosa yangu.
/: Sipo sipo hapa sipo
mbinguni ni ngome
ya moyo wangu.:/
2. Iache dunia,
uone ngome,
unapofurahishwa
moyo wangu.
Ni Yerusalemu
unaojengwa
na mawe mazuri
ya dhahabu tu.
/:Ndiko, ndiko,
ndiko ngome
na makimbilio
ya moyo wangu.:/
3. Mwangani kwa Yesu
ni raha tamu,
hakuna makosa
na shida huko.
Vinubi na sauti
za nyimbo nzuri
zinaufurahisha moyo
huko.
/:Raha, raha, raha
tamu
mbinguni kwa Yesu
naitamani.:/
Comments
Post a Comment