159.Mbinguni, Mbinguni
1. Mbinguni, mbinguni
Kuna mji mwema.
/:Wapendeza sana,
ni wake Mungu,:/
2. Milango ya mjini
ni dhahabu tu,
/: mungu ndiye jua
anaung`aza.:/
3. Ugonjwa hauko,
kufa hakuna.
/:Wenyeji wa humo
ni wa kweli tu:./
4. Waimba usiku
hata na mchana
/: Wakimsifu Bwana
Mungu wetu tu.:/
5. Wote waimbao
wana furaha.
/:Wang`azwa na damu
ya Bwana Yesu.:/
6. Vijana sikieni
wote kwamba.
/:Twapendwa na Yesu,
Bwana wa mbingu.:/
7. Twendeni kuingia
wote mjini,
/:Tupewe uzima
na Bwana wetu!:/
Comments
Post a Comment