167.Ni sikukuu Ile
1. Ni sikukuu siku ile ya
kumkiri mwokozi!
Moyo umejaa tele,
kunyamaza huwezi.
Siku kuu! Siku kuu!
ya kuoshwa dhambi
zangu kuu.
Hukesha na kuomba tu,
ananiongoza miguu.
Sikukuu! Siku kuu!
Ya kuoshwa
dhambi
zangu kuu.
2. Tumekwisha kupatana
mimi wake, Yeye wangu,
na sasa nitamwandama,
nikiri neneo la Mungu.
Siku kuu!...
3. Moyo tulia kwa Bwana
kiini cha raha yako,
huna njia mbili tena:
Yesu ndiye njia yako.
Siku kuu! …..
4. Nadhiri yangu ya mbele
nitaiweka daima,
hata ije siku ile
ya kuonana salama.
Siku kuu!
Comments
Post a Comment