158.Liko Pumziko la Mioyo
1. Liko pumziko la mioyo,
amka wee unayechoka
Unaugua kama mfungwa
kwa shida za moyo wako
Umtazame Kondoo wa
Mungu
atakuchunga kwa furaha
Uache mzigo enenda.
Vita nzuri yamalizika,
safari yabaki kidogo
inayokusumbiua mno.
2. Mungu ametuchagulia
pumziko lisilo mwisho
Amelitengeneza kale,
mtu hajazaliwa bado,
kufa kwa mfurahisha
Mponya,
tupate pa kupumzika.
Aita, anaalika
mioyo inayokaa na shida,
msikawie njooni leo!
Ingieni pumzikoni!
3. Ninyi mshindwao na
mzigo
mlemewao na uzito
Rukeni kimbieni hima,
tokeni pangoni mmwenu,
msienende kwa kuinama
Mponya anawaambieni:
Mimi ni pumziko lenu,
ninyi wana wote wa
Mungu.
Popote mwalizwa na shida,
kwa Yesu mwanyamza
kimya!
4. Hapo pumzikeni rahani,
wasi wasi hatunao.
Shikeni neno hili jema:
Pumzikeni Yesu yuko!
Shikeni mabawa upesi,
karukeni kama ndege
Wako jamaa wanangoja,
Furahi moyo, shangilia,
patana nao utukuze,
uko mwaka wa pumziko!
Comments
Post a Comment