148.Mungu Baba Mungu Mwana

1. W:Mungu Baba, Mungu
Mwana,
Mungu Roho, twakusifu  
twakushangilia sote,
umejifunua kwetu 
kwa upendo, 
kwamba wanadamu 
wakujue wote.
K:/:Mungu wetu
W:Anapenda tuwe 
   Wake
K: Dhambi zetu
W:Tuache, tumfuate.:/


2. W: Mungu Baba wewe 
 uliumba vyote,
Mbingu, dunia 
navilivyomo vyote, 
watu ndege na 
wanyama uliumba, Jua 
mwezi na nyota 
vyakutukuza.
K:/: Mungu wetu:/


3. W: Mungu Mwana, 
wewe ulikuja kwetu, 
ukaishi kama
 mwanadamu kweli,
 ukateswa na kubeba 
dhambi zetu,
 kwamba sisi tupate 
wokovu kweli.
K:/: Mungu Wetu:/


4. W: Mungu Roho, 
uliye kiungo chetu, 
wakusanya 
na kuita watu wote, 
tufundishe kumjua
Bwana wetu, 
na utukufu wake 
hata milele.
K:/: Mungu wetu:/



 

Comments

Popular posts from this blog

17. Tuimbe na kusifu

32 Kitoto Mpenzi Lala Wee

143.Mungu ni wa Utukufu