Tuimbe na kusifu Kwa nyimbo za furaha: Yesu Bwana wetu amezaliwa leo Zizini Bethlehemu. Furaha ya mioyo. Mponya na mwokozi, Tunakusifu 2. Nakutamani sana,
uliyetoka juu.
Ee Mwokozi mwema
tuliza moyo wangu,
unipe neema yako,
Kitoto cha huruma.
Univute juu, univute juu.
3. Rehema zake Mungu
ni nyingi, alimtuma
Mw/ana wake Yesu,
awakomboe watu,
atufanyie njia,
tufike tena kwetu.
Kwetu ni kwa Mungu,
kwetu kwa Mungu.
4. Na watu wakaao
katika giza wote
wanakungojea
Wewe Mwokozi wetu,
na kukufurahia
uliyetukomboa.
Yesu Bwana wetu twakutukuza.
Sauti: Kijerumani. T.B. 17, P. B. Ill 7.2, N.K. 30
Asili: Kadriga 1706
Mtunga maneno: Schubert, 1734-1791 Wimbo: Schlaf wohl, du Himmelsknabe du 1. Kitoto mpenzi lala wee,
Kitoto wa mbingu!
Malaika wakupepea
ulale kwa raha.
Nasi maskini wachunga
tunakubembeleza wee.
Lala, ulale: Kitoto wee, ulale.
2. Maria kwa upendo mkuu
amlaza vizuri.
Yosefu amekaa kimya
ili asimwamshe. Na wanyama wa nyumbani
wamenyamaza kabisa:
Lala, ulale: Kitoto wee, uiale.
3. Yesu utakapokua,
watakuumiza.
Kilimani pa Golgota,
utasulibishwa.
Kwa hiyo sasa lala tu!
Kwa raha na utulivu!
Lala, ulale: Kitoto wee, ulale.
1. Utukufu ni wa Mungu juu, tukuzo lote, uwezo wote ni wa Mungu, Bwana wetu, Bwana Wetu, Mungu ni wa pekee Shangilio lake Lijaze katika dunia popote, Jina lake litukuzwe na watu wote. Tumshangilie Mungu wetu na Bwana wetu nyimbo za tukuzo tumpeni heshima zote, tumwimbie, Sifa na tukuzo zampasa zote ni zake Mungu wetu!
Comments
Post a Comment