7. Moyo Wangu Sikiliza
Sauti na wimbo: Froehlich soil mein
Herze spingen. L. B. W. 46, P. B. 1163, N.K.
Mtunga sauti:LJ. Crueger, 1656,1598-
1662. Mtunga maneno: Paul Gerhardt,
1607-1676
1. Moyo wangu sikiliza,
habari njema hii,
ya wokovu mkubwa.
Sikia kuimba
kwao malaika na watu:
"Yesu azaliwa."
2. Mponya amekuja leo
kutoka mbinguni,
aokoe watu.
Mungu wetu ameshuka,
akawa mwana mtu
kwa ajili yetu.
3. Na sasa yumo zizini,
aita: "njooni,
hima kwangu wote,
Nawaondolea ninyi
uchungu wowote,
muwe na furaha"
4. Basi tumwendee hima
wakubwa wadogo,
njooni wote sasa!
Yule anayetupenda,
tumpende na sisi,
awe mwanga wetu.
5. Wenye shida na ukiwa njooni,
awape
neema yake Mungu,
Yeye ana mali nyingi,
dhahabu na fedha
za mioyo yenu.
6. Ninakaa ufimwenguni
lakini napenda
kuhamia kwako.
Mwisho niwe furahani
pamoja na Wewe,
ทาwenye utukufu.
Comments
Post a Comment