8. Amekuja Mwokozi
Sauti na wimbo: Kibena, T.M.3
1. K: /: Amekuja
W: Mwokozi.:/
K: /: Ufalme wa juu karibu.
W: Amekuja Mwokozi.:/
2. K: /: Geukeni
W: mioyo.:/
K: /: Watatupwa wenye kiburi.
W: Geukeni mioyo. :/
3. K /: Shoka lipo
W: Shinani,:/
K: /:Mti usiozaa wakatwa.
W: Shoka lipo shinani.:/
4. K: /: Ana ungo
W: mkononi, :/
K: kupepeta ngano yake.
W: Ana ungo mkononi.:/
5. K: /:Yatachomwa
W: Makapi,:/
K: Ngano
yawekwa chanjani.
W: yatachomwa makapi :/
6. K: /:Nabatiza W: kwa maji, :/
K: Yeye, hubatiza kwa Roho.
W: Nabatiza kwa maji. :/
7. K: /:Mbele yake şifa i, :/
W: Şifa i,:/
K: Kumfungulia viatu,
W: Mbele yake sifai. :/
8. K: /: Elekea
W: Mbinguni,:/
K: Kristo katufanyia Njia.
W: Ya kwendea
mbinguni.:/
Comments
Post a Comment