15. Tawi Limechipuka


Sautî na wimbo: Es ist ein
Ros'entsprun^en. P.B. I 228, LB. W. 58,
N.K. 13
Asili: Koeln. 1599


1. Tawi limechipuka
shinani mwa Yese,
kama tulivyopashwa
habari na wazee.
Likatoa ua
wakati wa usiku,
lilipochanua.


2. Isaya alitaja
ua hilo zuri.
Ni Yesu, Mponya wetu,
Maria alimzaa.
Usiku mtulivu.
Uwezo wake Mungu
umefanya hivi.

3. Na ua hili dogo
lanukia vyema;
lang'aa kama jua
giza lafukuzwa.
Ni Mwana wa Mungu
pia mwana Adamu;
Mwokozi wa watu.


4. Siku ya kufa kwetu Yesu
tuongoze, tuiache dunia,
twende furahani
mbinguni kwa Mungu
Pale tutakusifu
Pasipo kukoma.

Comments

Popular posts from this blog

17. Tuimbe na kusifu

32 Kitoto Mpenzi Lala Wee

143.Mungu ni wa Utukufu