6. Wakristo lwekeni Mioyo Tayari
Sauti: N.K. 164. Wimbo: Mit Ernst, o
Menschinkinder. P. B. 1 5 & 94
Mtunga maneno: V. Thilo, 1607-1662
1. Wakristo, iwekeni
mioyo tayari.
Yesu awaingie,
ni Mwokozi wenu.
Mungu amemtuma
kwa neema na rehema,
atuletee sisi
uzima na nuru.
2. Mwokozi anakuja,
mlimieni njia!
Mioyo iwe safi
acheni matendo
yanayomchukiza.
Lijazwe kila bönde,
milima ipunguzwe
mioyoni mwenu.
3. Ukiwa mnyenyekevu,
wapendwa na Mungu.
Ukiwa na kiburi,
utaangamizwa.
Ukimtumikia,
Mungu kwa mwendo
mwema
umpendezao yeye,
Yesu akupenda.
4. Uniweke tayari
niliye maskini,
Ee Yesu siku hizi
kwa rehema yako.
Ingia moyoni,
ukinijia sasa.
Nami nitakusifu
kwa kinywa na moyo.
Comments
Post a Comment