25 Mungu ni wa Utukufu

Sauti: Imechukuliwa kwa Cantate "Gott İst
Licht". Wimbo: Hark! The herald angels
sing.T.B. 15, N.K. 23, L.B.W. 60
Mtunga sauti: F. Mendelssohn, 1840
Mtunga maneno: Ch. Wesley, 1739

1. Mungu ni wa utukufu
panapo mbinguni juu,
na kwao wampendezao
duniani raha kuu.
Sikieni nchi zote
huko mjini Bethlehemu:
/: Kristo amezaliwa,
Bwana wetu daima. :/


2. Watu na malaika wote
wanamtukuza Yesu,
ashukaye toka mbingu
kuwa kama maskini.
Akaacha enzi yake,
akavaa unyenyekevu:
/: Kristo amezaliwa,..:/


3. Asifiwe Mungu Mwana
na Mwokozi wa watu,
mleta mwanga na uzima
Yesu mshinda kuzimu, Mfalme
wa utengemano
huko mjini Bethlehemu.
/:Kristo amezaliwa,...:/

Comments

Popular posts from this blog

17. Tuimbe na kusifu

32 Kitoto Mpenzi Lala Wee

143.Mungu ni wa Utukufu