4. Fungua Milango Yote

Sauti na wimbo: Macht hoch die Tuer P. B.
1226, N.K. 4, L.B.W. 32

Asi": J. A. Freylinghausen, 1704
Mtunga maneno: G. Weissel, is9o

1. Fungua milango yote,
yuaja Bwana wa mbingu.
Mfalme wa wafalme wote,
Mwokozi wa ulimwengu.
Atuletea uzima;
kwa hiyo tumwimbieni:
Tumsifuni Mungu,
aliyetuumba.


2. Ni mwenye haki na shujaa,
upole mwingi amevaa;
Rehema ni taji ya ke, huruma ni
fimbo yake:
Atuondolea shida.
Kwa hiyo tumwimbieni:
Tumsifuni Mungu,
Mwokozi wetu mkuu.


3. Miji na nchi huchipushwa
afikako Mfalme huyu;
nayo mioyo huchekeshwa
anayoingia Yesu.
Ndiye jua la furaha
linalotufurahisha.
Tumsifuni Mungu
mtunza mioyo yetu.


4. Fungua milango yote!
Tengenezeni mioyo!
Makuti yawe upole,
furaha, pendo, amani.
Mwokozi atawajia,
aleta raha, uzima.
Tumsifuni Mungu,
ni mwenye rehema.


5.Njoo, Mwokozi wangu Yesu, 
nakufungulia moyo. 
Uingie na rehema, 
nione upole wako.
 Uniongoze kwa roho, 
nifike kwako mbinguni, 
jina lako Bwana
 lisifiwe pote.

Comments

Popular posts from this blog

17. Tuimbe na kusifu

32 Kitoto Mpenzi Lala Wee

143.Mungu ni wa Utukufu