17. Tuimbe na kusifu


Tuimbe na kusifu
Kwa nyimbo za furaha:
Yesu Bwana wetu
 amezaliwa leo
Zizini Bethlehemu.
Furaha ya mioyo.
Mponya na mwokozi,
Tunakusifu


2. Nakutamani sana,
uliyetoka juu.
Ee Mwokozi mwema
tuliza moyo wangu,
unipe neema yako,
Kitoto cha huruma.
Univute juu, univute juu.


3. Rehema zake Mungu
ni nyingi, alimtuma
Mw/ana wake Yesu,
awakomboe watu,
atufanyie njia,
tufike tena kwetu.
Kwetu ni kwa Mungu,
kwetu kwa Mungu.


4. Na watu wakaao
katika giza wote
wanakungojea
Wewe Mwokozi wetu,
na kukufurahia
uliyetukomboa.
Yesu Bwana wetu twakutukuza.

Comments

Popular posts from this blog

32 Kitoto Mpenzi Lala Wee

143.Mungu ni wa Utukufu