42 llitoka Nuru Kuu
Never shone a light so fair
Mtunga maneno: J. F. Crosby 1823-1915
Asili:N.S56. Sauti:S.S&S. 2
Mtunga sauti: R. Lowry
1. llitoka nuru kuu,
kuliko nuru zote.
Na huo wimbo wa juu
wapita nyimbo zote;
Ndiyo habari tukufu,
ya Kristo wa utukufu,
awajia wapole;
Ni Mungu pamoja na sisi,
Imanueli.
2, Mwaka huandama mwaka,
wimbo huu na uimbwe;
Wapenda kukumbusha,
mzee na wanawe,
ndiyo habari tukufu,
ya Kristo wa utukufu,
awajia wapole;
Ni Mungu pamoja na sisi,
Imanueli
3. Twafurahi siku hii
ijavyo kila mwaka;
Nasi tufanye bidii
huku tukikumbuka,
Ndiyo habari tukufu,
ya Kristo wa utukufu,
awajia wapole;
Ni Mungu pamoja na sisi,
Imanueli.
Comments
Post a Comment