37 Sote Tufurahi

Asili: Kihaya, T.M 6
Mtunga maneno: W. Kyakajumba

1. K: Sote tufurahi,
W: habari ni njema
K: Njooni nyote wahi,
W: tupate uzima
Sasa yametimia
yaliyotabiriwa
Mwokozi kazaliwa.


2. K: Kule Bethlehemu
W: Yesu kazaliwa
K: Mama Mariamu
W: alivyoambiwa. Sasa ...


3. K: Kumbe, huyo Mwana
W: kalazwa horini
K: Huyo Yesu Mwana
W: akawa shidani. Sasa ...


4. K: Mwana atiiye
W: ni Bwana shujaa,
K: Kwake tuwe wana,
W: ni Mponya dunia. Sasa ...


5. K: Jeshi la mbinguni
W: katoa Injili.
K: Watu malishoni,
W: kaona ni kweli. Sasa ..

6. K: Mungu yupo nasi
W: katika dunia.
K: pendo kwa waasi,
W: katoa kwa nia. Sasa ...


7. K: Raha na tushike,
W: tunaye Masihi
K: Haya twende kwake
W: sauti zasihi. Sasa ...


8. K: Wote wenye Mwana
W: wanao uzima.
K: Yeye ndiye Bwana,
W: atoa karama. Sasa ...


9. K: Nyota yatunuka
W: shinani mwa Yese.
K: Bwana atukuka,
W: akatutakase. Sasa ...


10. K: Sasa, ndugu, nyote
W: tangaza neema.
K: Waje kwake wote
W: tupate rehema. Sasa ...

Comments

Popular posts from this blog

17. Tuimbe na kusifu

32 Kitoto Mpenzi Lala Wee

143.Mungu ni wa Utukufu