33. Niende na Wachungaji
Sauti na wimbi: Mit den Hirten will ich
gehen. Gr. M.H. I 39, N.K. 31
Mtunga sauti: A. Rische, 1891-1906
Mtunga maneno: E. Quandt, 1835-1911
1. Niende na wachungaji
nimtazame Mponya wangu,
kazaliwa duniani
kwa kunipenda mimi.
2. Nimwimbie na malaika,
niusifu utukufu.
Anautengemaza,
kila moyo umpende.
3. Nikawaze na Maria
jambo hili la ajabu:
Aacha mwili mzuri,
achukua wa kimtu.
4. Nimpelekee vipaji
na watambuzi wa nyota,
na nîmpe mali yangu,
hata uzima nimpe.
5. Nakupenda, u Mwokozi,
nikumbuke siku hii.
Uje mwangu moyoni,
uufanye kikao.
Comments
Post a Comment