28.Amkeni Upesi
Sauti: Kijerumani. Wimbo:
fhr Hirten erwact. T.B. 10, N.K. 26
Asili: Paderborn
1- Amkeni upesi wachunga
kondoo!
Malaika washuka,
habari watupa:
Furaha karibu,
Mwokozi aja!
2. Wachungaji njooni,
tumtafuteni!
Akiwa zizini pigeni filimbi.
Furaha karibu...
3. Wachungaji hima washika njia.
Pamoja wamwona
mamaye, babaye.
Furaha karibu ...
4. Wamjua upesi mtoto wa
mbingu.
Wapiga magoti
kumwimbia nyimbo.
Furaha karibu ...
Comments
Post a Comment